MSANII wa
muziki wa kizazi kipya Bongo, Baby Joseph Madaha amenusurika kubakwa
nchini Kenya baada ya kupanda jukwaani akiwa ametinga kivazi cha nusu
utupu.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Bongo, Baby Joseph Madaha akipozi.
Tukio hilo lilitokea Jumamosi iliyopita
katika mji wa Naivasha uliopo Nairobi nchini humo ambapo mwanadada huyo
alipopanda jukwaani akiwa amevaa sketi fupi iliyokuwa imeacha sehemu
kubwa ya mapaja wazi, wanaume wakware walianza kumvutia chini kwa nguvu.
Baby Madaha akifanya shoo na kunengua jukwaani akiwa ametinga sketi fupi.
“Nusura Baby Madaha abakwe, wanaume
wakware walishindwa kuvumilia, palepale jukwaani wakaanza kumvuta huku
wengine wakimng’ang’ania paja lake lakini aliokolewa na mabaunsa
vinginevyo tungekuwa tunaongea mengine,” kilisema chanzo.
Baby madaha akizidi kuwapagawisha wakenya.
Paparazi limezinasa picha kadhaa
zinazomuonesha Baby Madaha akiwa anang’ang’aniwa na wanaume tofauti huku
wengine wakimchungulia sehemu zake ‘muhimu’ pamoja na kumshika mapaja
yake.
Wanaume wakiung'ang'ania mguu wa Baby madaha.
“Kweli ilikuwa ni hatari siku hiyo maana wanaume waliniganda balaa kila nilipokuwa naimba jukwaani walikuwa wakinivutia kwa
huku chini walikokuwa wamesimama lakini niliokolewa na mabaunsa, hata hivyo shoo ilikuwa na mzuka sana,” alisema Baby Madaha.
Baby Madaha akipata akiwa na baadhi ya mastaa kutoka Kenya.
Kwenye shoo hiyo iliyokuwa na nyomi ya
kutosha, Baby Madaha alikamua vilivyo sambamba na wasanii wakali kutoka
Kenya akiwemo Jua Kali na Wayree.
Post a Comment