Waziri
wa Maliasili na Utalii Mh. Razalo Nyalandu akipongezana na Balozi
Chales Sanga Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Utalii
Tanzania TTB mara baada ya kuzindua rasmi SITE ya Maonyesho ya Kimataifa
Utalii ya Tanzania yanayojulikana kama Swahili International Tourism
Expo (SITE) kwenye hoeli ya Serena Mwisho ni mwa wiki, Maonyesho hayo
yatakayohusisha kampuni binafsi, taasisi za kiserikali kama Bodi ya
Utalii Tanzania (TTB) pamoja na washirika wengine katika sekta hiyo
yanatarajiwa kufanyika tarehe 1 mpaka 4 Oktoba, mwaka huu katika ukumbi
wa Mlimani City Dar es Salaam, Katikati ni Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya
Utalii Bi. Devotha Mdachi.
Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Razalo Nyalandu akizungumza katika uzinduzi huo wakati alipokuwa akisoma hotuba yake.
Wageni waalikwa mbalimbali wakiangalia jinsi mabanda yatakayotumiwa na washiriki wa maonyesho yatakavyokuwa.
Balozi
Chales Sanga Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Utalii
Tanzania TTB akimkaribisha Waziri Razalo Nyalandu ili azungumze na kisha
kuzindua maoyesho hayo.
Seraphin Lusala Mkurugezni wa Masoko na Mauzo Serena Hotel kulia akiwa katika hafla hiyo.
Balozi
Chales Sanga Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Utalii
Tanzania TTB kulia akiwa pamoja na wageni wengine katika hafla hiyo.
Wageni waalikwa mbalimbali wakifuatilia mambo mbalimbali yaliyokuwa yakiendelea wakati wa hafla hiyo.
Waziri
wa Maliasili na Utalii Mh. Razalo Nyalandu akiwa pamoja na Kaimu
Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii TTB Bi. Devotha Mdachi na kulia ni Beatrice
Mwiru Ofisa Masoko wa bodi hiyo.
Msanii Wanne Star kushoto na kundi lake wakitoa burudani katika hafla hiyo.
Burudani kutoka kundi la Wanne Star ikiendelea wakati wa hafla hiyo
Meneja
wa Masoko Bodi ya Utalii Tanzania TTB Bw. Geofrey Meena Katikati,
Emmanuel Okware Meneja wa mauzo kutoka Qatar Airways kulia na mdau Juma
Mabakila wakiwa katika hafla hiyo.
Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Razalo Nyalandu akizungumza na Bi. Lima D'Silva Mwakilishi wa mauzo Ethiopian Airlines.
Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Razalo Nyalandu akisalimiana na wageni mbalimbali waliohudhuria katika hafla hiyo.
Baadhi ya wanahabari wakiwa katika hafla hiyo
Wageni waalikwa wakibadilishana mawazo katika hafla hiyo
Mkuu
wa Kitengo cha Uhusiano Bw. Goefrey Tengenea wa pili kutoka kulia akiwa
katika picha ya pamoja na maofiza wenzake wa TTB wakati wa hafla hiyo.
Napenda
kuchukua nafasi hii kutoa shukrani zangu za dhati, kwa wageni wote
mliofika katika tukio hili muhimu ambapo nitatambulisha kwenu kuanzishwa
kwa onesho jipya la utalii la kimataifa litakalojulikana kwa jina la
Swahili International Tourism Expo (S!TE).
Sekta ya
Utalii ni kichocheo kikubwa cha ukuaji wa uchumi hasa kwa kuchochea
ukuaji wa sekta nyingine za kiuchumi kama vile usafirishaji, viwanda na
biashara, kilimo, sanaa za mikono na kadhalika. Sekta ya utalii ina
uwezo wa kuongeza ajira kwa haraka zaidi na inatambulika kwamba kila
mtalii mmoja anapokuwa nchini huchangia takribani nafasi 12 za ajira za
aina mbalimbali.
Aidha, Utalii
ni tasnia muhimu katika kuongeza kipato na kupunguza umasikini, kukuza
mahusiano ya kijamii na vile vile katika kutunza na kuendeleza maeneo ya
kihistoria na maliasili.
Hapa nchini,
katika kipindi cha kati ya mwaka 2002 na 2013, utalii wa kimataifa
umekuwa kwa zaidi ya asilimia 50%, kutoka watalii 575,000 mwaka 2002
wambao waliliingizia taifa Dola za Marekani milioni 730 hadi kufikia
watalii 1,135,884 mwaka 2013 ambao waliingizia taifa Dola za marekani
Bilioni 1.81.
Tanzania
imebarikiwa kwa kuwa na vivutio vya maliasili na utamaduni vya kipekee.
Kutokana na kuwepo kwa vivutio hivi, taasisi ya Kimataifa ya World
Economic Forum katika taarifa yake ya ushindani kwenye tasnia ya Utalii
(Travel and Tourism) imeitaja Tanzania kuwa ni nchi ya pili (2) duniani
ikiongozwa na Brazili kwa kuwa na mazingira asilia yenye Urithi asilia
wa kimataifa, wingi wa wanyamapori na ardhi kubwa iliyo hifadhiwa.
Hakika, ni
ukweli usiopingika kwamba katika vivutio saba vya maajabu ya asili
katika bara la Afrika, vitatu vinatoka Tanzania. Huu ni ushuhuda kwamba
juhudi zetu za kuhifadhi mazingira zinazaa matunda. Hivi sasa Bonde la
Ngorongoro; hifadhi ya Taifa ya Serengeti, na Mlima Kilimanjaro ni
vivutio ambavyo vimeorodheshwa katika Maajabu saba ya asilia barani
Africa.
Hata hivyo,
hatuwezi kutegemea tu uwingi na ubora wa vivutio hivi vya utalii peke
yake. Ni muhimu kuongeza juhudi zaidi kuliko wakati mwingine wowote, ili
kujenga uelewa wa utajiri huu kidunia. Kama taifa, tunahitaji juhudi na
mikakati zaidi ili kutangaza vivutio vyetu.
Kwa
kuzingatia umuhimu wa kuendelea kutangaza utalii wetu na kuifaya
Tanzania iweze kushindana kimataifa, mnamo mwezi Februari, 2013, Bodi ya
Utalii Tanzania (TTB), iliingia makubaliano na kampuni inayojulikana
kama Pure Grit Project and Exhibition Management LTD, hapo mwanzo
ilijukana kama Witch & Wizard Creative (Pty Ltd) ili kuanzisha
maonyesho ya utalii ya kimataifa nchini Tanzania yajulikanayo kama
Swahili International Tourism Expo -S!TE), ambayo yataanza rasmi Mwezi
Oktoba, 2014.
Pure Grit
Project and Exhibition Management LTD ni kampuni inayoendesha maonesho
ya utalii ya INDABA ambayo ni maonesho ya tatu kwa ukubwa duniani.
Onesho la S!TE litafanyika hapa Dar es salaam, mwezi Oktoba kila mwaka
katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani City na kujikita zaidi katika
kuvutia washiriki kutoka ndani nan je ya nchi.
Mkoa wa Dar
es Salaam umechaguliwa mahsusi kuwa eneo la kufanyika kwa onesho la S!TE
kutokana na sehemu ulipo Mkoa huo kijiografia, na uwepo wa miundombinu
bora na huduma nzuri zinazofaa kwa kuendesha au kuanzisha maonyesho ya
utalii ya kimataifa.Hadi kufikia Juni 2014, hali ya maandalizi ya onesho
hili ni kama ifuatavyo.
Mwenendo wa
idadi ya washiriki hadi sasa: Zaidi ya asilimia 50% ya nafasi za
maonesho hayo tayari zimejazwa kwa kuchuliwa na makampuni binafsi na
Bodi za Utalii za nchi mbalimbali. Aidha, kuna idadi kubwa na ya
kuridhisha ya maombi ya washiriki inayoendelea kuandaliwa. Lengo ni
kwamba ifikapo katikati ya mwezi Agosti, 2014 tuwe tumetumefikia
asilimia 100.
Programu
maalum ya kuwaleta nchini wakati wa maonesho hayo mawakala wakubwa wa
biashara ya Utalii: Katika kuhakikisha kuwa onesho hili linakuwa ni
fursa ya kuwaunganisha wafanyibiashara ya Utalii wa Tanzania na masoko
ya Utalii, S!TE itakuwa na programu maalum (Hosted buyer and travel
writer programme) ya kuwaleta nchini wakati wa maonesho hayo mawakala
wakubwa wa biashara ya Utalii na waandishi wa habari za utalii (Tour
Operators, Wholesalers,
Packagers and
Travel Agents and Travel Writers) na kuwapangia ratiba maalum ya
kuonana na washiriki wa maonesho hayo ili kuwawezesha kuanzisha uhusiano
wa kibiashara. Mawakala hao wapatao ishirini na wandishi wa habari kumi
watagharimiwa (hosted) na S!TE.Hadi kufikia Juni 2014,mawakala 13
kutoka Marekani, Australia, Ujerumani, Uholanzi, India, Mexico, Norway
na China wamethibitisha ushiriki wao.
Utangazaji wa Onesho la S!TE: Onesho la S!TE lina tovuti ijulikanayo kama www.site.co.tz.
Tovuti hii imeandaliwa ili kukidhi maudhui ya onesho lenyewe ambapo
inataarifa nyingi zinazoweza kumfanya yeyote anayetembelea tovuti hiyo
kupata taarifa zote muhimu kwa muda mfupi.
Kwa mfano
tovuti inatoa taarifa za ukumbi wa onesho, mabanda ya maonesho
yatayojengwa na kumruhusu mteja kuchagua eneo kulingana na uwezo wake.
Aidha, tovuti hii ambayo pia imeunganishwa na ukurasa wake wa Facebook,
inapatikana kwa lugha mbalimbali
Pamoja na
kuitangaza Tanzania kama kituo muhimu cha utalii katika ukanda wa Afrika
ya Mashariki, S!TE ina lengo la kuunganisha wafanya biashara wa Utalii
wadogo na wa kati wa Tanzania (Small and Medium Tourism Enterprises -
SME’s), na masoko ya utalii ya kimataifa.
Ni ukweli
kwamba SME’s za kitanzania zina uwezo mdogo wa kimtaji wa kuweza kufikia
masoko ya utalii ya kimataifa. Kupitia S!TE, hasa kupitia programu
maalum ya kuwaleta nchini wakati wa maonesho hayo mawakala wakubwa wa
biashara ya Utalii, itasaidia katika kutatua changamoto hii.Naomba
watanzania kuchangamkia fursa hii muhimu katika kukuza biashra ya Utalii
nchini.
Post a Comment