Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

Lulu Michael: Sina muda wa kumbembeleza Mwanaume coz wanaonitongoza kwa siku ni wengi hata siwezi kuwahesabu.



Wakati  wanawake  wengine  wakionekana  kubembeleza  penzi  na  kujinyenyekeza  kwa  wapenzi  wao ili wasiachike,  Lulu  Michael  anasema  hana  muda  huo  kwani uzuri  wake  unatosha  kuwavuta  wanaume  wa  kila  aina  kutoka  katika  kila  kona  ya  Tanzania.....
Lulu  amedai  kuwa  inawezekana  mwanaume  wa  kwanza  kwake  ndo  chaguo  lake  namba  moja, lakini  suala  la  kuanza  kulilia  mapenzi  au  kuumia  halipo  na  kamwe  hawezi  kufanya  hivyo.

"Mapenzi  ni  magumu  hasa  kwetu  sisi  wasanii. Kuna  wanaume  wanaweza  kuja  kwako  ukadhani  ni  wema  lakini  baada  ya  kumaliza  haja  zao  huwaoni, ndo  maana  huwa  sioni  haja ya  kujilizaliza  kwa  mwanaume  coz  akigundua  umezimika  ndo  kabisa  atakugeuza  Toilet paper ya kuchambia......

"Najua  wapo  wengi  sana  wanaonitamani, lakini  kwa  taarifa  yao  ni  kwamba nipo  makini  sana  na  naitambua  thamani  yangu." Alisema  Lulu.

Hata  hivyo  Lulu  alisema  kuwa  huwa  anatongozwa  na  wanaume  wengi  sana  kutokana  na  uzuri   alionao, hali  inayomfanya  abadili  namba  ya  simu  kila  mara  kukwepa  usumbufu.

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright BONGO HABARI
Back To Top