Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

UCHAWI WA ‘SHUKURANI’ KATIKA MAPENZI-4

 
Wiki iliyopita niliishia pale mama Shebby akiwa nyumbani kwake saa 3:24 aliposhika simu yake akakuta SMS mbili zilizotoka kwa Pascal waliyekutana supermarket, akamnunulia deodorat  mbili. Moja ya SMS hiyo ilimuuliza kama alilala na ya mwisho alimfahamisha deodorat aliyomchangulia mkewe aliipenda. Unajua kiliendelea nini? Ungana nami...

 
 “Haraka sana nilimjibu kwa kumwandikia SMS mbili, ya kwanza nilimjulisha sijalala, ispokuwa nilikuwa bize na mipangilio ya nyumbani nikiwa kama mama wa familia, ya pili ilijusu hisia zangu kwamba nilifurahi mwanamke mwenzangu kufurahia deodorant ambazo nilichagua kupitia kwa mumewe.
“Hapohapo Pascal alinitumia SMS akaniambia mume wangu ananijali kwa sababu ameninunulia gari la kutembelea, nikamjibu hajaninunulia, lile ni lake isipokuwa huwa nalitumia katika siku ambazo mume wangu anakuwa hana mizunguko mingi ya kikazi.
“Pamoja na hivyo, Pascal aliniandikia SMS akizidi kumsifia mume wangu kwamba ananijali, akasema wanaume wengi hawawapi wake zao magari. Sijui kwa nini maneno hayo hayakunizindua na kunifanya niheshimu mchango wa mume wangu katika maisha yangu.
 
“Katika nyakati ambazo huwa nakiri kuwa Shetani ana nguvu sana ni hapa, kwani niliendelea kujilegeza kwa SMS mbele ya Pascal mpaka mwenyewe nahisi aliona namtaka, maana kesho yake ya pili alinipigia simu akinitaka anitoe lunch, nami sikupinga na huo ndiyo ukawa mwanzo wa usaliti.
“Vilevile huo ulikuwa mwanzo wa kujilaumu kwani hakuna kitu kizuri ambacho nilikipata zaidi ya kupakwa na kunukishwa shombo nje ya ndoa. Mwanaume ambaye nilimpandisha thamani mbele ya mume wangu hakuwa lolote wala chochote, tamaa zilinipeleka pabaya sana.
“Siku niliyokutana naye faragha kwa mara ya kwanza, nilijuta kwani nilivyofikiria kwamba alikuwa na vitu vya ziada kumpita mume wangu hakuwa hivyo.
“Nafsi ilinisuta kwa kuvunja nadhiri niliyoiweka ya kutomsaliti mume wangu ambaye nina historia naye ndefu ya tulikotoka hadi kuamua kuungana na kuwa mwili mmoja.
“Ingawa kwa utashi wangu niliamua kufanya hivyo, niliumia zaidi kufuatia kumvulia nguo Pascal na kumkaribisha maungoni mwangu, nilijiona mkosaji sana!
“Tangu siku hiyo niliapa kutorudia tena usaliti kwa sababu hauna maana yoyote zaidi ya kumkosesha mtu husika amani na furaha.
“Kila nilipomtazama mume wangu nilihisi alikuwa akijua nilimsaliti, nilitamani kujiweka huru kwa kumwambia nilichepuka kutoka njia kuu, lakini nilisita na kubaki nikijihukumu moyoni kwa upuuzi nilioufanya,” mama Shebby alihuzunika.

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright BONGO HABARI
Back To Top