Msimamizi
wa Mashindano ya Tanzania Movie Talents, Bw Tony Akwesa akitoa
maelekezo kwa washiriki waliojitokeza kwaajili ya shindano la Tanzania
Movie Talents kwa kanda ya Pwani unaoendelea kufanyika katika Ukumbi wa
Makumbusho ya Taifa, Jijini Dar Es Salaam. 
Baadhi
ya washiriki wakiwa kwenye mstari tayari kwa kuchukua fomu za ushiriki
wa shindano la Tanzania Movie Talents lililoanza rasmi leo Kwa Kanda ya
Pwani.

Washiriki waliojitokeza kuchukua fomu za Shindano la Tanzania Movie Talents wakisoma fomu kwa umakini kabla ya Kujaza.

Washiriki wakipewa maelekezo na Mmoja wa wafanyakazi wa Proin Promotions.

Washiriki wakisoma fomu kwa makini.

Wakielekezwa Kujaza Fomu za ushiriki wa Shindano la Tanzania Movie Talents.
Shindano la Tanzania Movie Talents limeanza rasmi leo Katika Kanda
ya Pwani Ambapo usaili unaendelea kufanyika leo na kesho katika Ukumbi
wa Makumbusho ya Taifa uliopo Jijini Dar Es Salaam ambapo takriba
washiriki zaidi ya 250 wameweza kuchukua fomu za ushiriki wa Shindano
hilo.
Shindano hili ni muendelezo wa shindano la kusana vipaji vya
kuigiza ambalo limefanyika tayari kwa Kanda Tano za Tanzania yaani Kanda
ya Ziwa, Kanda ya Kati, Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Kanda ya Kusini
na Kanda ya Kaskazini na sasa tunamalizia Kanda ya Pwani ambapo washindi
watano watapatikana kwa Kanda ya Pwani na kila mmoja atajinyakulia
kitita cha Shilingi Laki Tano taslimu.
Shindano hili limelenga kuibua vipaji vilivyojificha ambavyo havikuwahi kupata nafasi ya kuonekana.
Baada ya Wasindi watano kupatikana kwa Kanda ya Pwani, washindi
takribani 20 kutoka kanda zote sita za Tanzania watawekwa katika kambi
moja Jijini Dar Es Salaam na watapewa mafunzo kutoka Kwa Walimu Wa Sanaa
kutoka Chuo Cha Sanaa cha Bagamoyo na baadae kushindanishwa na hatimaye
mshindi mmoja kupatikana na Kuibuka na zawadi nono ya Shilingi Milioni
50 za Kitanzania.
Vilevile Washiriki kumi watakaopatikana katika fainali hiyo
watakuwa chini ya Kampuni ya Proin Promotions na watatengeneza filamu ya
pamoja na hatimaye Kuweza kunufaika na Mauzo ya Filamu hiyo
Post a Comment