KIFO cha msanii wa filamu, Rachel Haule kimewaumiza wengi lakini
baadhi yao ni wasanii wenzake, Halima Yahaya ‘Davina’ aliyeachiwa
hausigeli wa marehemu katika mazingira ya ajabu huku Wastara Juma
akiumizwa na viatu na pochi alivyopewa na Rachel kabla hajafariki dunia.
Msaniii wa Bongo Movie Halima Yahaya ‘Davina’ akiwa na simanzi kubwa.
Akizungumza na Ijumaa juzi, Davina alisema alihangaika sana
kumtafutia Rachel hausigeli ili atakapojifungua asipate shida lakini
siku moja kabla ya kifo, alipompigia simu akitaka ampelekee mtu wake
simu haikupokelewa hadi alipopata taarifa za kifo.
“Aliniambia nimtafutie msichana, nikafanya hivyo, wakati najipanga
kumpelekea nyumbani kwake nasikie eti kafariki, naumia sana,” alisema
Davina.
Naye
Wastara alisema: “Nilikutana naye wiki chache zilizopita, nikaipenda
pochi yake, akaniambia atanipa. Siku iliyofuata akaniletea na viatu, leo
naambiwa hatunaye, mbona hivi vitu vitanitesa sana!”
Get Free Email Updates to your Inbox!
Post a Comment