STAA wa filamu Bongo, Yusuf Mlela ametoa kioja cha aina yake baada ya
kufunguka kuwa akifika hatua ya kuingia kwenye ndoa anataka mwanamke
atakayemzidi umri.
Yusuf Mlela.
Tofauti na vijana wengine ambao wanapenda kuoa wake wadogo kwao,
Mlela alisema anaamini mwanamke akimzidi umri ndoa itadumu na maisha yao
yatakuwa mazuri kwani atakuwa tayari ameshakomaa kiakili na atakuwa na
uwezo mkubwa wa kuiendesha familia.
“Nahitaji mwanamke anayenizidi umri na sitaki nimzidi mimi naamini
huyo tutaelewana na ndoa itadumu, sitaki mwanamke ninayemzidi umri mimi
maana itakuwa shida kwani sijapangilia hivyo,” alisema Mlela.
Get Free Email Updates to your Inbox!
Post a Comment