MSANII wa filamu Bongo, Elizaberth Michael ‘Lulu’ hivi karibuni
aliwashangaza watu baada ya kuvukwa na gauni alilokuwa amevaa na
kulazimika kutembea huku sehemu kubwa ya kifua chake ikiwa wazi.
Msanii wa filamu Bongo, Elizaberth Michael ‘Lulu’.
Tukio hilo lilitokea hivi karibuni katika kiwanja kimoja kichopo
mjini Arusha ambapo mmoja wa watu aliyemtia machoni Lulu aliyeomba
hifadhi ya jina lake alisema:
“Yaani nilimuona Arusha akiwa amevaa gauni lililoacha wazi matiti
yake, kaficha chuchu tu na inavyoonekana gauni lilimvuka, akaonekana
akihangaika kulirudishia bila mafanikio.”
Ijumaa
lilimtafuta Lulu kupitia simu yake ya mkononi bila mafanikio ila
juzikati akatundika picha kwenye mtandao wa instagram akiwa amevaa gauni
kama lile aliloonekana nalo Arusha.
Get Free Email Updates to your Inbox!
Post a Comment