IMEKAA poa sana! Lile bifu lililotia fora kwa wasanii wa filamu,
Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ na Yobnesh Yusuf ‘Batuli’ huku kila mmoja
akiapa kutopatana na mwenzake, hatimaye limekwisha siku chache baada ya
kifo cha msanii mwenzao, Adam Philip Kuambiana.
“Steve na Batuli kwa sasa wameshamaliza tofauti zao, wamepatana, wanaelewana vizuri sana na ni baada ya kifo cha Kuambiana ndipo walikaa wakaamua kuzungumza na kumaliza tofauti zao,” kilisema chanzo hicho.
Baada ya kunyetishiwa ishu hiyo, Ijumaa Wikienda liliwasaka wahusika ambapo Batuli alithibitisha kwamba ni kweli amemaliza tofauti zake na Steve na sasa wameanza maisha mapya kwani amegundua maisha ni mafupi na kifo kinakuja muda wowote.
Kwa upande wa Steve Nyerere alikuwa na haya ya kusema: “Mimi ndiye Mwenyekiti wa Bongo Movie Unity na nilishasema nitamaliza tofauti zote yaani mabifu yote yataisha kwa sababu mimi ni kiongozi na mfano wa kuigwa nimemaliza bifu na Batuli naamini na hayo mengine yataisha, huu ni mwanzo tu.”
Wasanii wa filamu, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ na Yobnesh Yusuf ‘Batuli’ wakiwa katika picha ya pamoja.
Kwa mujibu wa chanzo makini, wawili hao walimaliza tofauti zao
kutokana na kifo cha ghafla cha Kuambiana hivyo wakaamua wenyewe
kuyamaliza kwani wameona maisha ni mafupi.“Steve na Batuli kwa sasa wameshamaliza tofauti zao, wamepatana, wanaelewana vizuri sana na ni baada ya kifo cha Kuambiana ndipo walikaa wakaamua kuzungumza na kumaliza tofauti zao,” kilisema chanzo hicho.

Post a Comment