STAA wa sinema za Kibongo, Halima Yahaya ‘Davina’ amefunguka kifo cha
mwigizaji Adam Kuambiana kinampa majonzi zaidi kila anapofikiria muvi
waliyocheza kwa mara mwisho na marehemu.
Staa wa sinema za Kibongo, Halima Yahaya ‘Davina’ akiangusha kilio katika msiba wa Kuambiana.
Akieleza masikitiko yake, Davina alisema kabla Kuambiana hajapatwa na
umauti, waliigiza naye sinema ya Stupid Farther na Who is My Son akiwa
na Mtitu (William) ambazo zote bado hazijatoka.
“Yaani
hata siamini Kuambiana ametutoka kabla hata muvi tulizocheza naye
hazijatoka, ameondoka wakati bado tunamhitaji jamani!” alisema Davina
huku akilengwalengwa na machozi.
Get Free Email Updates to your Inbox!
Post a Comment