Kijana anatakiwa kupata elimu ya afya hasa wale wanaoshindwa kupata huduma ya afya ya uzazi na kujikuta wamepata magonjwa ya zinaa ambayo husababishwa na ngono zembe, alisema.
Alisema lengo la mkutano huo ni kutoa elimu, kujenga uhusiano na jamii na kuangalia jinsi watakavyoweza kufikisha ujumbe kwa vijana husika.
Kawala alisema mikakati waliyojiwekea ni kuhusisha jamii na wazazi kuhakikisha vijana wanalelewa katika mazingira stahiki ikizingatiwa malezi ya mtoto huanzia katika ngazi ya familia.
Hata hivyo, alisema Serikali imefanya juhudi mbalimbali kuhakikisha afya ya uzazi kwa kijana inaangaliwa na inapewa kipaumbele.
Kawala alisema taarifa iliyotolewa mwaka 2005-2012 inasema ngono kwa kijana mara nyingi inafanyika kabla ya ndoa kwa kijana wa kike na wa kiume.
“Asilimia 10 ya vijana wanafanya ngono katika umri wa miaka 15 na aslimia 43 katika umri wa miaka 18 na robo yao tu wanasema wametumia kondomu,” ilisema taarifa hiyo.
Post a Comment