Kama umeshushwa thamani unakuwa kwenye hatari ya kuachwa.
Hata kama mwenzako alikuwa ameshafikiria suala la kuingia kwenye ndoa na wewe
lakini kwa sababu ameshakushusha thamani ndoa inaweza kuyeyuka.
Ukiwa kwenye ndoa ni hatari zaidi maana mwenzako
hukuchukulia wa kawaida – mazoea huzidi na hapo ndipo uhitaji wa kuwa na
mwingine wa pembeni unapoanzia. Haoni cha muhimu tena kwako, ndiyo maana wazo
hilo huvamia ubongo wake kwa kasi sana.
Itafikia hatua, kama upo ndani ya ndoa, mwenzako atagoma
kuongozana na wewe na kama ikitokea hivyo mkikutana na rafiki zake njiani
hatakutambulisha. Hisia kwamba hamuendani humwingia.
UNAFANYAJE SASA?
Kubwa unalotakiwa kufahamu rafiki yangu mpendwa, suala la
kupanda au kushuka thamani lipo mikononi mwako. Yapo mambo ambayo
ukiyazingatia, mwenzako hawezi kukuchoka na kufikia hatua ya kukushusha
thamani.
Tayari tumeshaona athari zake lakini hapa sasa nataka kukupa
mbinu ambazo ukiwa nazo makini basi itakuwa rahisi kwako kubaki namba moja na
mtu muhimu zaidi (ndiyo inavyotakiwa kuwa) kwa mpenzi wako maana ni haki yako.
ANZIA MWANZO
Ni rahisi zaidi kulinda thamani yako kuanzia mwanzo wa
uhusiano wenu. Ikiwa tayari mmeshakomaa halafu tatizo hilo likajitokeza,
hutumika nguvu nyingi zaidi kulirekebisha kuliko kujizatiti kuanzia mwanzo wa
uhusiano. Ni mambo gani hayo? Twende hapo chini.
CHUNGA KAULI ZAKO
Naomba ieleweke wazi kuwa mada hii ni maalum zaidi kwa
wanawake. Kitu muhimu cha kwanza kabisa kwa mwanamke ambaye anataka kuilinda
thamani yake kwa mpenziwe ni kupima sana kauli zake.
Acha kuropoka hovyo, pima maneno yako na ikiwezekana kama
unadhani kuna jambo huna uhakika nalo usizungumze kabisa. Katika eneo hili, uwe
makini zaidi mnapokuwa na watu wengine. Kama mwanamke usiwe mchangiaji hoja
sana.
Utulivu wako unaweza kuwa silaha kubwa ya kukufanya ubaki na
thamani yako kama mwanamke anayejitambua.
USIRUHUSU MAPENZI
Msichana mwenye kujitambua na kufahamu thamani yake sawasawa
hawezi kuruhusu mwili wake ujulikane na mwanaume harakaharaka. Onesha
unajitambua na usikubali kirahisi kuuacha mwili wako uchezewe.
Mpe hoja; kwanza mapema, hajakuoa wala kukuchumbia, haraka
ya nini? Wakati unawaza kuhusu kutoa penzi lako, lazima ufikirie kuhusu athari
zinazoweza kukupata kwa kukurupukia mapenzi. Mwanaume ambaye bado
hamjachunguzana na huna uhakika naye wa kutengeneza maisha, kichwani mwake
hakuweki kwa asilimia kubwa.
Ukumbuke kwamba, ukipata matatizo yoyote – binafsi au
yanayosababishwa na uhusiano wenu, anakuwa hana uwajibikaji wa asilimia kubwa
kwa tatizo hilo. Utabaki wewe na matatizo yako!
Post a Comment