Serikali
imeombwa kufuata nyayo za serikali ya Uganda chini ya Rais Yoweri
Museveni kwa kuktaa kuruhusu ushoga licha ya kuziudhi nchi za magharibi
zinazokingia kifua vitendo hivyo.
Ombi
hilo limetolewa na Imamu wa Msikiti wa Mwembechai, Sheikh Mohammed
Muhenga, alipokuwa akiwahutubia waumini kabla ya swala ya Ijumaa
iliyoswaliwa msikiti hapo, jijini Dar es Salaam.
Imamu
Muhenga alisema kitendo cha Watanzania kunyamazia na kukumbatia matendo
maovu yanayomchukiza Mungu vinaweza kuzua balaa kwa taifa.
“Tushirikiane
kukemea maovu, tusinyamazie matendo yanayomchukiza Mungu kwani hakuna
anayeweza kuhimili ghadhabu za Mungu akiamua kutuadhibu,”alisema .
Sheikh
huyo alisema vitendo vya ulevi, biashara ya watu kujiuza, ujambazi na
matendo mengine kwa kisingizio cha kukabiliana na hali ngumu ya maisha
vinapaswa kuepukwa kwa nguvu zote.
Sheikh
alisema matendo vya ushoga na maovu mengine ni kuvuka mipaka kwa
wanadamu ya uumbaji na humchukiza Mungu, hivyo ni wajibu wa kila mtu
kukemea na kuyakataa matendo hayo.
Hivi
karibuni Uganda ilipitisha sheria kali dhidi ya vitendo vya ushoga na
kukera nchi ya Marekani na washirika kwake ambao wameruhusu vitendo
hivyo katika nchi zao licha ya kwenda kinyume na mafundisho ya kidini.
Post a Comment