Mtangazaji aliyewahi kuwa mpenzi wa mwanamuziki Nasibu Abdul,
‘Diamond’, Penniel Mungilwa ‘Penny’ ameibuka na kusema kuwa anashukuru
amepata mchumba ila suala la ndoa siyo la leo wala kesho.
Mtangazaji aliyewahi kuwa mpenzi wa mwanamuziki Nasibu Abdul, ‘Diamond’, Penniel Mungilwa ‘Penny’.
Akipiga stori na Ijumaa juzikati, Penny alisema wengi wamekuwa
wakitaka kusikia suala la yeye kuolewa baada ya kubainika ana mchumba
lakini mwenyewe anasema hajafikiria hilo la kuitwa mke kwa sasa.
“Kwenye hilo la kufunga ndoa naweza kusema bado niponipo sana, yapo
mambo yangu ambayo lazima niyakamilishe kabla ya kuolewa, ndoa si
mchezo, kujipanga ni muhimu,” alisema Penny.
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI
Get Free Email Updates to your Inbox!
Post a Comment