Mwanasheria wa Serikali, George Masaju.
Mwanasheria
wa Serikali, George Masaju, na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya
Wilaya ya Hai, Kilimanjaro, Meleckzedeck Humbe, wamepandishwa kizimbani,
wakikabiliwa na mashtaka ya ukiukwaji wa sheria na taratibu za uchaguzi
wa Serikali za Mitaa wa Desemba 14, mwaka jana.
Masaju
na wenzake, wanakabiliwa na kesi namba 04 ya mwaka 2015 iliyofunguliwa
na Gerald Mlay katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Hai, akipinga
matokeo yaliyotangazwa na kumpa ushindi mpinzani wake, Peter Mshiko
(CCM) ambaye ni Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Orori, Kata ya
Narumu.
Mwanasheria
Mkuu pamoja na Mkurugenzi wa Wilaya ya Hai, waliwakilishwa na Wakili wa
Serikali, Leah Kimaro, ambaye alimwomba Hakimu Mkazi Mfawidhi, Denis
Mpelembwa, kumpa siku 14 za kuandika majibu ya shtaka linalowakabili.
Kwa
mujibu wa wakili huyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Hai,
hajampa taarifa ya kimaandishi kuhusu uchaguzi unaodaiwa kutokuwa huru
na haki.
“Ikikupendeza
mheshimiwa, naomba nitoe udhuru wa Mkurugenzi wa Upepelezi wa Makosa ya
Jinai nchini (DPP), kwamba hakuweza kufika mahakamani hapa kutokana na
sababu zilizo nje ya uwezo wake, lakini pia naomba mahakama yako tukufu
inipe muda wa siku 14 za kuandika majibu,” alidai wakili huyo. Baada ya
ombi hilo, Hakimu Mpelembwa alisema kwa kuwa upande wa Jamhuri, umeomba
muda wa kuandika majibu, mahakama, hivyo mahakama imeridhia na kwamba
kesi hiyo itatajwa tena Februari 16, mwaka huu.
Mbali
na kesi hiyo, Humbe na baadhi ya wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi huo,
bado wanakabiliwa na kesi nyingine tano za uchaguzi zilizofunguliwa
mahakamani hapo.
Kwa mujibu wa kalenda ya mahakama hiyo, atapandishwa tena kizimbani Februari 5, mwaka huu.
Mara
baada ya kuahirishwa kwa shauri hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa
Halmashauri ya Wilaya ya Siha, Rashid Kitambulilo na wenzake wawili, nao
walipandishwa kizimbani, wakikabiliwa na kesi namba 06 ya mwaka 2015 ya
ukiukwaji wa taratibu na kanuni za uchaguzi wa serikali za mitaa wa
Desemba 14, mwaka 2014.
Walalamikaji
katika kesi hiyo, Richard Maly na wenzake 44 ambao ni wanachama wa
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Wilaya ya Siha ambao
wamefungua kesi, wakidai uchaguzi huo uligubikwa na ukiukwaji mkubwa wa
taratibu za uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI
Post a Comment