Mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Kilondo Ludewaa.
Mbunge Filikunjombe akisisitiza jambo wakati akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kilondo.
Mwenyekiti
wa kata ya Kilondo wa Chadema Bw Edgar Kyula akimpongeza mbunge wa
wa Ludewa Deo Filikunjombe kushoto wakati wa mkutano wake kijijini
Kilondo
Mbunge
Filikunjombe akikabidhi nyavu za kuvulia samaki kwa ajili ya vikundi
vya vijana wote Kijiji cha Kilondo na Lusisi Ludewa.
Mbunge
Filikunjombe wa tatu kulia akiwa na viongozi wa kijiji cha Kilondo na
Lusisi ambao aliwapa nyavu na vifaa vya michezo.
Kikongwe
mkazi wa kijiji cha Kilondo akisalimiana na mbunge wa Ludewa Deo
Filikunjombe baada ya kumalizika kwa mkutano wake kijijini hapo.
Mtaalam
wa umeme akimuelekea mbunge Filikunjombe mambo ya kitaalam baada ya
kutembelea maporomoko ya mto Makete ambao utatumika kuzalisha umeme
kushoto ni katibu wa mbunge Filikunjombe Bw Stany Gowele.
Mbunge Filikunjombe akitazama mto Makete.
Mbunge
wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe (kulia) akiwa katika box huku
ameshika tama eneo la kando ya ziwa nyasa juzi alfajiri akisubiri
usafiri wa bodi kuelekea Matema wilayani Kyela baada ya kufanya ziara
ya siku mloja kijijini Kilondo wengine pichani ni mkurugenzi wa
kampuni ya Kilondo Investment Bw Erick Mwambeleko wa pili kushoto
,katibu mwenezi mkoa wa Njombe Honolatus Mgaya na katibu mwenezi wilaya
ya Ludewa Bw Felix.
Na matukiodaimaBlog
WANANCHI
wa kijiji cha KIlondo kata ya Kilondo wilayani Ludewa mkoani Njombe
wamempongeza mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe kwa kuwa
mbunge pekee katika jimbo hilo kufika kulala chini ardhini kwenye
nyumba isiyo na mlango wala dirisha (Pagale) katika kijijini hicho
toka nchi ipate uhuru wake mwaka 1961.
Mbunge Filikunjombe
na msafara wake wa watu zaidi ya 15 walifika katika kijiji
hicho cha Kilondo kilichopo mwambao mwa ziwa nyasa kwa lengo la
mbunge huyo kuwaanzishia mchakato wa kupatiwa umeme kupitia
shirika lisilo la kiserikali la Kilondo Investment linalofadhiliwa na
mradi wa usambazaji vijijini (REA)
Akizungumza kwa
niaba ya wananchi wa kijiji hicho mwenyekiti wa serikali ya
kijiji hicho Bw Laurian Kyula alisema kuwa jimbo hilo limepata
kuwa na wabunge zaidi ya 5 ila hakuna mbunge ambae alifika na
kukubalia kulala katika kijiji hicho kutokana na kuwa na miundo
mbinu mibovu na kutokuwa na nyumba ya kisasa ya kulala wageni zaidi
ya nyumba za wananchi ambazo nyingi zipo kienyeji zaidi hazina
hadhi .
" Kweli tumeshindwa
kuamini kuona mbunge anaamua kulala kijiji hapa hata bila kuwepo
kwa maandalizi mazuri ya kulala ......tumekuwa na wabunge wengi sana
ila wapo baadhi yao hata kukejeli kuwa kijiji hakina hadhi ya
kulaza waheshimiwa hadi watakapoboresha mazingira...kati ya viti
ambavyo hatukupata kufikiria ni pamoja na kuja kupokea mgeni wa
kiwilaya kuja kulala hapa kijijini ila wewe mheshimiwa wetu
Filikunjombe umekuwa ni kiongozi wa aina yake" alisema mwenyekiti
huyo
Akimpongeza mbunge huyo kwa jitihada zake za
kuwasogezea huduma ya umeme kijijini hapo mwenyekiti huyo
alisema kijiji hicho ni moja kati vijiji ambavyo vipo mwambao mwa
ziwa nyasa na uwezekano wa kuunganishwa na umeme wa gridi ya
Taifa kutoka Ludewa mjini ama Kyela mkoani Mbeya ni vigumu kutokana
na kuzungukwa na milima na maji hivyo kwa upande wao waliamini
kabisa kamwe hawatakuja fikiwa na huduma za umeme.
" Tunashindwa kujua
ni kiasi gani mbunge wetu unavyotuhangaikia kwa mambo ambayo
wengine waliotangulia walituhakikishia kuwa ni vigumu kufikiwa na
huduma ya umeme kwa kuwa ni porini labda hadi tutakaposogea karibu na
vijiji vya nje ya Mwambao kauli ambazo vilitufanya kukata tamaa
kabisa kwa umeme kwetu ni huduma isiyo wezekana.....ila tunashangazwa
leo kupitia mbunge wetu Jembe Filikunjombe unatuletea wataalam wa
kuanza kujenga mradi wa umeme hapa kijijini"
Bw Kyula alisema
kati ya mambo ambayo wao hawata kuja kusahau maishani mwao ni
utendaji kazi wa mbunge huyo na maendeleo makubwa aliyoyafanya katika
jimbo hilo la Ludewa kwa kipindi cha miaka minne ya ubunge wake
huku wapo waliokaa miaka mitano bila kufanya jambo linaloonekana
kwa wananchi wao.
Hivyo alisema iwapo chama cha mapinduzi (CCM)
kitataka kulipoteza jimbo hilo la Ludewa ni pamoja na kujaribu
kufanya maamuzi yasiyo hitajika kwa wananchi yakiwemo ya kukata jina
la mbunge wao katika mchakato wa kuomba kugombea ubunge jimbo
hilo la Ludewa na kumpa nafasi mtu wa kwao watashangazwa na maamuzi
magumu ya wananchi kwa kulitoa jimbo hilo upinzani kama fundisho kwa
CCM kupenda wanachopenda wao na sio wananchi.
Awali mkurugenzi
mtendaji wa mradi wa Kilondo Investment Bw Erick Mwambeleko akielezea
mradi huo alisema kuwa mpango wa kuwaunganisha wanakijiji hao na
umeme ulikuwepo toka wakati mbunge Profesa Raphael Mwalyosi akiwa
madarakani ila cha kushangaza kila alipomfuata kutaka kusaidia
kufanikisha kuanzishwa kwa mradi huo aliishia kutoa kauli za
kukatisha tamaa kuwa haweza kusaidia kupeleka umeme kijijini hapo
kwa kuwa ni gizani sana hakuna faida yoyote .
" Ni kweli kijiji hiki cha Kilondo kipo porini zaidi
ila kuna watu wanaishi hata mimi Mwambeleko ni mzaliwa wa hapa
hivyo nimesoma sayansi na kutumia elimu yangu nikaona ngoja
nishirikiane na mbunge Filikunjombe kuleta ukombozi wa umeme huku
kwa kupitia kampuni yangu ya Kilondo Investment kampuni ambayo mchango
wa mbunge ni mkubwa zaidi hadi leo tunaanza mchakato wa kuleta umeme
hapa....
Alisema kuwa tayari fedha kiasi cha zaidi ya Tsh
milioni 300 zimepatikana kwa ajili ya kuanza utekelezaji wa mradi huo
ambapo fedha hizo kiasi zimetoka REA na nyingine ni fedha ambazo ni
mchango wa mbunge Filikunjombe .
Pia alisema umeme huo utazalisha kijijini hapo
kupitia maporomoko ya maji ya mto Makete ambayo yanaingia katika ziwa
nysa na kuwa maporomoko hayo yana nguvu ya kuzalisha umeme KV 50 na
kasi ya maji katika maporomoko hayo ni lita za ujazo 9312 kwa sekunde
maji ambayo yanatosha kabisa kwa uzalishaji wa umeme wa kutosha kaya
zote kijijini hapo na kijiji cha jirani.
Kwa upande wake mbunge Filikunjombe akielezea sababu
ya kulala kijijini hapo alisema kuwa moja kati ya ahadi yake kwa
wananchi wa Ludewa ni kufikisha maendeleo kila kona ya jimbo hilo na
kuwa akiwa katika ziara pale ambapo jua litazamia ndipo atakapolala
bila kujali uwepo wa maandalizi ama lah.
"Wananchi wote wa Ludewa ni wapiga kura wangu hivyo
imekuwa ni kawaida yangu kuwa nao wakati wote na kulala popote na
kula chochote ambao wao wanakula siku zote .....hivyo jua
linapozamia nikiwa ziarani nitalala hapo bila kujali maandalizi lengo
kuona nashirikiana na wananchi wangu kwa mazingira yoyote
yale......nimefurahi sana leo kulala katika nyumba hii inayojengwa
ambayo haina sakavu ,milango wala madirisha (Pagale) mimi ni siufanyi
ubunge kama ufalme kuwa nikija mimi ziarani wananchi wangu wasumbuke
kufanya maandalizi yasiyo ya kawaida"
Kuhusua mradi huo wa umeme Filikunjombe alisema kuwa
lengo lake kuona wananchi hao wanapatiwa umeme mapema zaidi
ikiwezekana ndani ya mwaka huu wananchi hao waweze na umeme katika
makazi yao hivyo kuwaomba wananchi kutoa ushirikiano kwa mafundi
waliofika kijijini hapo kuanza utekelezaji wa mradi huo pamoja na
kuwasaidia kufanya tathimini ya mahitaji ya taa na ufungaji umeme
katika nyumba zao.
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI
Post a Comment