Ishu hiyo ilijiri nyumbani kwa mastaa hao eneo la Ifitedunu, Jimbo la
Anambra nchini humo Ijumaa iliyopita ikiwa ni siku 65 tangu mzee huyo
alipofariki dunia baada ya kufanyiwa oparesheni ya goti alipodondoka
kwenye ngazi nyumbani kwake maeneo hayo.
Wakina P-square wakiwa na wake zao katika msiba huo.
Tofauti na ilivyozoeleka kwamba kwenye msiba watu huwa wanalia na
kuomboleza, mazishi hayo yaliyohudhuriwa na mastaa kibao nchini humo
yalikuwa tofauti kwani watu walikuwa na nyuso za tabasamu huku
wakiserebuka na matarumbeta juu.
Ulinzi mkali ukiimarishwa katika msiba huo.
Mbali na kuonekana kuwa kama sherehe, pia mazishi hayo yaliripotiwa
kuwa ya gharama zaidi kuanzia jeneza lililobeba mwili wa baba yao, gari
‘spesho’ lililokuwa na jina la Dady badala ya namba za usajili na
wahudhuriaji waliopiga sare nyeupe huku wakijifotoa picha wakicheka na
kutupia kwenye mitandao ya kijamii.
Mwili wa baba wa P-Square ukiwa kwenye jeneza.
Pia kivutio kikubwa kilikuwa ni wake wa mastaa hao ambao walipewa
ulinzi mkali uliowekwa katika mazishi hayo yaliyohudhuriwa kwa mualiko
maalum.
Baba wa P-Square (aliyenyosha mikono) enzi za uhai wake.
Cha kushangaza, wakati mwili wa baba yao ukiwa mochwari, jamaa hao
walidaiwa kuendelea na ratiba za kimuziki huku wakifanya shoo kama kawa
jambo ambalo kwa Bongo haliwezekani.Kwa sasa mastaa hao hawana mzazi hata mmoja baada ya mama yao naye kufariki dunia mwaka 2012.
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI
Post a Comment