Unapofikiria wachezaji wanaoongoza kwa kasi wakiwa uwanjani kwenye ligi kuu ya soka nchini England mara moja majina yatakayokujia kichwani ni ya watu kama Raheem Sterling , Gabriel Agbonlahor na Alexis Sanchez
Wachezaji hawa wamezoeleka kuwatisha mabeki kwa kasi yao wakiwa uwanjani jambo ambalo limekuwa msaada mkubwa sana kwa timu zao ambazo zimefaidika kwa mabao yatokanayo na sifa ya wachezaji hawa kuwa na uwezo wa kukimbia kwa kasi ya ajabu .
Kiukweli wana kasi kama ionekanavyo lakini hawajamzidi kiungo Mfaransa wa Newcastle United Mousa Sissoko .
Kiungo huyu wa klabu ya Newcastle United alionekana kuwa na kasi ya ajabu wakati takwmu zilipoonyesha kuwa alikimbia kwa kasi ya kilomita 35.3 kwa saa kwenye mechi kati ya timu yake na Leicester City ambapo Newcastle ilishinda 1-0, kasi ambayo ndio kubwa kuliko wachezaji wote kwa msimu huu kwa mujibu wa takwmu rasmi .
Kwa kawaida Sissoko hajazoeleka kuwa na kasi kubwa na aliwashangaza wengi kwa jinsi takwimu zilivyomuonyesha kuwa na kasi kuwaliko watu kama Wilfred Zaha na wengine wengi .
Wachezaji wengine walioonekana kuwa na kasi kubwa ni kiungo wa West Brom Cristian Gamboa , Eric Dier wa Tottenham na Raheem Sterling wa Liverpool ambao wana kasi ya kukimbia umbali wa kilomita 35 kwa saa .
Alexis Sanchez wa Arsenal ameingia kwenye orodha hii lakini amezidiwa na Gabriel Agbonlahor na Ross Barkley pamoja na Diego Costa wa Chelsea .
Wachezaji wanaoongoza kwa kasi kwenye kila timu ligi ya England 2014-15 | ||||
Mchezaji | Timu | Mpinzani kwenye mechi ya takwimu | Tarehe | Kasi (kph) |
Alexis Sánchez | Arsenal | Newcastle United | 13/12/2014 | 34.6 |
Gabriel Agbonlahor | Aston Villa | Southampton | 24/11/2014 | 34.8 |
Marvin Sordell | Burnley | Everton | 26/10/2014 | 34.0 |
Diego Costa | Chelsea | Liverpool | 08/11/2014 | 34.7 |
Wilfried Zaha | Crystal Palace | Stoke City | 13/12/2014 | 35.2 |
Ross Barkley | Everton | Swansea City | 01/11/2014 | 34.9 |
Ahmed Elmohamady | Hull City | Everton | 03/12/2014 | 34.6 |
Marcin Wasilewski | Leicester City | Queens Park Rangers | 29/11/2014 | 35.1 |
Raheem Sterling | Liverpool | Queens Park Rangers | 19/10/2014 | 35.0 |
Sergio Agüero | Manchester City | Tottenham Hotspur | 18/10/2014 | 34.7 |
Luke Shaw | Manchester United | Chelsea | 26/10/2014 | 34.2 |
Moussa Sissoko | Newcastle United | Leicester City | 18/10/2014 | 35.3 |
Yun Suk-Young | Queens Park Rangers | Manchester City | 08/11/2014 | 34.7 |
Nathaniel Clyne | Southampton | Stoke City | 25/10/2014 | 34.2 |
Erik Pieters | Stoke City | West Bromwich Albion | 28/12/2014 | 34.5 |
Connor Wickham | Sunderland | Aston Villa | 28/12/2014 | 34.5 |
Jefferson Montero | Swansea City | Everton | 01/11/2014 | 34.5 |
Eric Dier | Tottenham Hotspur | Liverpool | 31/08/2014 | 35.0 |
Cristian Gamboa | West Bromwich Albion | Leicester City | 01/11/2014 | 35.0 |
Stewart Downing | West Ham United | Tottenham Hotspur | 16/08/2014 | 35.1 |
Nyuma ya N’zonzi yuko kiungo wa Chelsea Cesc Fabregas ambaye ukiachilia mbali pasi 14 za mwisho kwa wafungaji wa Chelsea alizotoa ameweza kukimbia umbali wa kilomita 225.3 na anafuatiwa na Cristian Eriksen wa Tottenham Hotspurs ambaye amekimbia umbali wa kilomita 222 umbali ambao ni sawa na mbio tano tofauti za marathon.
Jina la Robin Van Persie limetokea kwenye orodha hii katika hali ambayo itashangaza wengi akiwa amecheza jumla ya mechi 13 pekee ambazo amemaliza dakika 90 ambapo ameweza kukimbia umbali wa kilomita 187.1 na amewazidi Yaya Toure wa Manchester City na Paul Konchesky wa Leicester City ambao wamekimbia umbali wa kilomita 179.7 na 173.1 katika mpangilio .
Wachezaji wanaoongoza kwa kukimbia umbali mrefu ligi ya England 2014-15 | ||
Mchezaji | Timu | Umbali aliokimbia (km) |
Mathieu Flamini | Arsenal | 191.0 |
Aly Cissokho | Aston Villa | 190.4 |
George Boyd | Burnley | 213.2 |
Cesc Fàbregas | Chelsea | 225.3 |
Joel Ward | Crystal Palace | 205.3 |
Gareth Barry | Everton | 198.2 |
Jake Livermore | Hull City | 218.2 |
Paul Konchesky | Leicester City | 173.1 |
Jordan Henderson | Liverpool | 204.8 |
Yaya Touré | Manchester City | 179.7 |
Robin van Persie | Manchester United | 187.1 |
Jack Colback | Newcastle United | 221.4 |
Steven Caulker | Queens Park Rangers | 187.4 |
Graziano Pellè | Southampton | 199.8 |
Steven N’Zonzi | Stoke City | 227.1 |
Sebastian Larsson | Sunderland | 209.1 |
Ki Sung-Yueng | Swansea City | 220.8 |
Christian Eriksen | Tottenham Hotspur | 222.8 |
Craig Gardner | West Bromwich Albion | 196.2 |
Aaron Cresswell | West Ham United | 211.5 |
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI.
Post a Comment