Mshambuliaji mpya wa Atletico Madrid Fernando Torres anaweza kuwa
bado hajaanza kuitumikia klabu yake lakini tayari ameshaanza kuvunja
rekodi tofauti tangu usajili wake toka Ac Milan ulipokamilika .
Utambulisho wake mbele ya mashabiki ndani ya uwanja wa Vicente
Calderon ulikusanya mashabiki 45,000 idadi ambayo haijawahi kuonekana
katika utambulisho wa mchezaji raia wa Hispania .
Mashabiki
wa Atletico Madrid wakinunua jezi za Fernando Torres siku chache baada
ya mshambuliaji huyo kutambulishwa kama mchezaji mpya wa Atletico.
Jezi namba 19 ambayo Fernando Torres amekabidhiwa hadi sasa inafanya
vizuri sana sokoni ambapo mashabiki wa Atletico Madrid wamekuwa
wakiinunua kama njugu ambapo ndani ya siku ya jumapili pekee duka rasmi
la klabu hiyo jijini Madrid liliuza jezi 200o ambayo ilikuwa rekodi
nyingine ikiwekwa na mshambuliaji huyo .
Fernando Torres aliwahi kuwa mchezaji wa Atletico Miaka kadhaa
iliyopita na mashabiki hawajaridhika kuvaa jezi yake ya zamani bali
wamesisitiza kununua jezi yake mpya ambayo atakuwa anaivaa katika
kipindi hiki .
Torres anatarajiwa kuanza kuitumikia Atletico Madrid kwenye mchezo
dhidi ya Real Madrid utakaopigwa hapo kesho katika michuano ya Copa Del
Rey.
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI.
Get Free Email Updates to your Inbox!
Post a Comment