Huenda utakuwa ni mwaka wa neema kwa
mshambuliaji Mbwana Samatta wa TP Mazembe kwa kuwa timu nne za Ulaya
zimeonyesha nia ya kumchukua.
Habari za uhakika zimelifikia gazeti hili
kuwa, timu nne kati ya hizo ambazo ni kutoka katika nchi za Ufaransa na
Italia, zimeonyesha nia ya kufanya kazi na mshambuliaji huyo Mtanzania.
“Kweli tunayajua majina ya timu nne, kumekuwa
na mawasiliano kupitia meneja wake Tanzania pamoja na uongozi wa TP
Mazembe,” kilieleza chanzo kutoka Ufaransa.
“Tusingependa kuanza kueleza kila kilichopo kwa sasa, lakini tunaamini Samatta anaondoka Mazembe msimu huu.”
Baada ya taarifa hizo, juhudi zilifanyika kumpata meneja wake, Jamal Kisongo ambaye alitoa ushirikiano.
“Kweli kuna timu zinamhitaji, kama
nilivyokueleza awali Mbwana si mtu wa kwenda kufanya majaribio, badala
yake kujiunga na timu na kuanza kazi.
“Sasa kinachofanyika ni taratibu na nimekuwa
na mawasiliano na uongozi wa TP Mazembe, hivyo vuteni subira kidogo,”
alisema Kisongo akionyesha kujiamini kuhusiana na mchezaji wake huyo.
Samatta yupo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mapumziko na amekuwa mchezaji tegemeo wa kikosi cha Mazembe.
Awali ilielezwa, mmiliki wa TP Mazembe, Moise
Katumbi, alikuwa akifanya juhudi kuhakikisha Samatta anabaki
Lubumbashi, DR Congo, lakini Kisongo amehakikisha anakwenda mbele zaidi
ili kupata mafanikio zaidi
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI.
Post a Comment