STAA
wa muziki na filamu Bongo, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ amewavaa baadhi ya
watu wanaoponda kitendo cha yeye kukubali kuvishwa pete ya uchumba na
mpenzi wake wa siku nyingi, Naftal Mlawa ‘Nuh Mziwanda’ kwa maelezo kuwa
ni kama maigizo kwani ndoa hakuna.
Staa wa muziki na filamu Bongo, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ akionyesha pete aliyovishwa na mpenzi wake Nuhu Mziwanda.
Akipiga stori na paparazi wetu, Shilole alisema anawashangaa
wanaodhani ataishia kuitwa mchumba tu bila kuiona ndoa, akasema
anachojua ndoa itafungwa siku si nyingi kwani wanapenda kwa dhati
“Kama ilishindikana kwao ni kwao tu, sisi ni watu wazima tunaojielewa
na mpaka hapa tulipofikia hakuna kitakachoharibika. Tunapendana hivyo
panapo uzima Mungu akijaalia ndoa itafungwa,” alisema Shilole.
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI.
Get Free Email Updates to your Inbox!
Post a Comment