Utakuwa mtu wa ‘hakuchi kunakucha’. Waswahili wanasema ‘bora liende’. Maisha yako yanakuwa hayana uelekeo, yanajipangia yenyewe namna yanavyotaka na wewe unakuwa mtu wa kufuatisha kama vile bendera inavyofuata upepo.
Mbali na kwenye maisha, tafsiri na kuweka nia ina maana kubwa sana hata kwenye ulimwengu wa wapendanao. Ndugu zangu, kila kitu lazima uweke nia kwanza.Lazima ujiwekee malengo, jenga picha ya aina ya uhusiano wako. Unataka kufikia katika hatua gani?
Jiulize unataka kuishi katika penzi ambalo halina mbele wala nyuma? Unataka kuishia katika penzi ambalo ni la ‘u-girl friend na uboy-friend’ miaka yote? Unataka kuishi penzi la ‘kumalizana leoleo tu’.
Una mpango wa kufikia hatua ya ndoa au pengine huna mpango kabisa, suala la kuwa bibi na bwana harusi kwako limekupitia kushoto.
Naamini jibu unalo moyoni lakini kwa kuwa mwaka ndiyo kwanza unaanza
kuyoyoma, leo ni tarehe 10 ya mwezi wa kwanza, hujachelewa.Unaweza
kufanya kitu na majibu yake utaanza kuyaona ndani ya mwaka huu na
pengine yanaweza kuwa na manufaa katika maisha yako.
Najua watu wengi huwa furaha yao ni kuona siku moja wanafikia kwenye
hatua ya ndoa lakini ili ufike huko zipo hatua mbalimbali ambazo mtu
unapaswa kuzipitia ili uweze kufikia hatua hiyo, twende pamoja katika
makala haya kuzifahamu zaidi:JIFUNZE ULIKOTOKEA
Huu ni mwaka mpya, unapaswa kutafakari, kule ulikotokea (mwaka jana na miaka iliyopita) ulikuwa kwenye mikono salama. Uliye naye ana mtazamo wa aina gani juu ya penzi lako? Kama mmepisha mawazo katika aina ya maisha yenu, unapaswa kujiuliza ulishawahi kuchukua hatua gani ili wote mbaki kwenye mstari mmoja?
Kama ulichukua hatua za kujaribu kumuelewesha mwenzako kwa njia ya kistarabu, ikashindikana, je umechukua hatua gani? Unakubali kuishi katika penzi la gizani?
Unaishi na mwenzako kimazoea, penzi ambalo halina mbele wala nyuma litakufaa mpaka lini? Jibu utakuwa nalo, chukua hatua!
TATIZO SUGU
Kwenye safari yako na umpendaye, unapaswa kuangalia katika miaka yote ambayo mmekuwa wapenzi, tatizo sugu ni lipi. Kikwazo katika kufikia kilele cha uhusiano wenu ni nini? Kama kikwazo ni dini au kikwazo ni ndugu je, umechukua hatua gani kuhakikisha suala hilo linaondoka.
Marafiki zangu, hakuna haja ya kupoteza muda mrefu wakati ukweli ni kwamba katika uhusiano wenu kuna kikwazo kikubwa ambacho kati yenu mmeshindwa kukikabili.
Itaendelea wiki ijayo siku ya Jumamosi.
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI.
Post a Comment