Staa wa filamu za Kibongo Vanitha Omary.
Ijumaa: Kuna hizi tetesi kwamba huyu mume wako wa sasa alikuwa ni
mpenzi wa rafiki yako Joan Matovolwa lakini wewe ukampora na mkaishia
kuoana, hili unalizungumziaje? Vanitha: (Kicheko) Ukweli ni kwamba mimi
na Joan ni marafiki wakubwa na hilo unaloongea halina ukweli wowote.
Maneno hayo yaliibuka baada ya kuwepo taarifa kuwa nataka kuolewa.Ijumaa: Wewe ni msanii lakini ni mke wa mtu, siku ukiwa hujaenda kwenye shughuli zako za kisanii uwapo nyumbani huwa unafanya nini? Vanitha: Huwa napenda kupikapika. Wewe ni mke wa mtu halafu ni sanii, je unapokuwa nyumbani unapenda kumpikia chakula gani mumeo?
Vanitha: Nikiwa nyumbani napenda kumpikia baby wangu chakula kizuri ambacho ni kipya. Ijumaa: Je, pale unapokuwa faragha na mumeo unapenda kumtega kwa vivazi gani?Vanitha: Ukweli huwa simtegi kwa mavazi, napenda kumtega kwa kukaa mtupu kwani wakati huo huwa ni wake, kwa nini nimfichie mali zake?
Ijumaa: Ni upi ugonjwa wako uwapo faragha na huyo mumeo?
Vanitha: Napenda sana kumkumbatia na yeye anikumbatie. Kale kajoto kanakotokea huku tukinong’onezana maneno matamu mimi nabaki kusinziasinzia.
Ijumaa: Watu wanasema wanaume hawatabiriki kwa kuchepuka, hivi siku
ukimfumania mumeo utafanya nini?Vanitha: Naomba Mungu isitokee kwani
nahisi nitafanya tukio baya na kumuacha siwezi, dah! Nahisi kutetemeka
ukiniambia hivyo.
Vanitha Omary akipozi.
Ijumaa: Mastaa wana skendo ya kuchukua waume za watu, wewe
unamlindaje mumeo asinaswe na wezi hao? Vanitha: Siwezi kusema
nitamlinda kwani sijui mtu anakuwa na nia gani na atakuwa amejipanga
vipi ila nabaki kumuomba Mungu amuepushe mume wangu na vishawishi.Ijumaa: Kuna wanawake ambao eti wanaona kuwapa waume zao mapenzi kinyume na maumbile ndiyo kuwashika, wewe kwako likoje hili? Vanitha: Mungu aniepushie mbali kwani ni jambo baya sana, sijawahi na sitowahi, nawaomba wanaofanya hivyo kuacha kwani Mungu hapendi.
Ijumaa: Ni kitu gani kimewahi kukufurahisha katika maisha yako?
Vanitha: Nilifurahi sana siku niliyofunga ndoa na mume wangu kwani tulipitia mikikimikiki mingi. Tumekaa kwenye uchumba kwa muda mrefu.
Ijumaa: Siku uliyohuzunika sana unaweza kuikumbuka?
Vanitha: Ni siku bibi yangu alipofariki, nakumbuka nilikuwa katika wakati mgumu kwani yeye ndiye alikuwa mlezi wangu na nilikuwa na ujauzito.
Ijumaa: Mbali na sanaa, ni kazi gani unaifanya?
Vanitha: Mimi ni mbunifu wa kupamba nyumba, nafanya kazi ya kuwadizainia watu nyumba zao kwa mapambo mpaka muonekano mzima wa nyumba .
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI
Post a Comment