MKURUGENZI Mtendaji wa Benchmark Production ambao ni
waandaaji wa Shindano la Bongo Star Search, Rita Paulsen ‘Madame Rita’,
amesema baada ya kushindwa kufanyika mwaka jana, zoezi hilo litafanyika
mwaka huu, tena kwa ufanisi mkubwa.
Akizungumza na gazeti hili mwanzoni mwa wiki, Madame Rita alisema 2014 ulikuwa ni mwaka wenye matukio mengi ya kimataifa yakiwemo Kombe la Dunia, lakini hata hivyo, kitu kikubwa kilichochangia kutofanyika kwa shindano hilo ni wafadhili wao, Zantel kushindwa kusema kwa wakati kuhusu kutoendelea kwao na mkataba.
“Mkataba wetu na Zantel uliwapa wao nafasi ya kwanza ya kuamua kujitoa au kuendelea, sasa baada ya mkataba wa awali kumalizika, wakachelewa kutuarifu na hata walipokuja kusema, muda ulishapita hivyo tukashindwa. Lakini mwaka huu tunawahakikishia mashabiki kuwa shindano hili litafanyika na litaboreshwa kuliko mara zote tangu lianzishwe,” alisema.

USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI.
Post a Comment