UKATILI, Mtoto mchanga ambaye anasadikika kuwa wa siku saba, amekutwa akiwa ameuawa na mwili wake kuwekwa kwenye mfuko wa rambo kisha kutupwa pembeni mwa jalala. Tukio hilo lilitokea hivi karibuni katika Mtaa wa Kaloleni katika Mji wa Tunduma katika Wilaya ya Momba, mkoani Mbeya .
Wakizungumza na gazeti hili mashuhuda ambao hawakupenda majina yao kuandikwa gazetini walisema kuwa walimkuta mtoto huyo akiwa amenyongwa kisha kuwekwa kwenye karatasi ya naironi (rambo) .
Waliongeza kuwa mtoto huyo alitambulika
baada ya watoto wadogo wakiwa katika michezo yao katika maeneo yao
kuuona mfuko huo wa rambo na kuufungua ndipo wakatoa taarifa wa wazazi
wao,” alisema mmoja wa wazazi wa eneo hilo.
Hata hivyo, aliyefanya kitendo hicho cha kikatili hakuweza kutambulika mara moja.
Wakithibitisha habari hiyo, kiongozi mmoja wa polisi katika kituo kidogo cha Tunduma alisema ni kweli kimetokea na mwili huo wa mtoto huyo umepelekwa katika hospitali ya serikali iliyopo mjini hapa kwa ajili ya uchunguzi.
“Tunaomba wenye kujua aliyefanya haya atuletee jina ili tumkamate,” alisema ofisa huyo bila kutaja jina lake kwa kuwa siyo msemaji wa polisi. Msemaji wa jeshi hilo mkoani Mbeya ni SACP Ahmed Msangi (pichani).
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI
Post a Comment