Japo familia hii ni maarufu lakini sio tajiri kama ambavyo watu wanaweza kudhani wakilinganisha umaarufu na ukubwa wan chi anayoiongoza Malkia Elizabeth na uwezo wa kiefedha .
Familia ya kifalme inayoongoza taifa la Lichtenstein ndio inayoongoza kwa utajiri ikiwa na utajiri wa paundi bilioni 4.9.
Ikiongozwa na Prince Hans-Adam II , familia hii ina utajiri ambao hauna uhusiano wowote na kodi za wananchi wa taifa dogo la Lichtenstein na utajiri walio nao kina Hans-Adam II unatokana na kampuni ya LGT Holdings ambayo inajiendesha kwa faida kubwa tofauti na familia nyingine za kifalme ambazo zina utajiri unaotokana kwa kiasi kubwa na kodi za wananchi wao .
Prince Hans-Adam II ndiye kiongozi wa kifalme tajiri kuliko wote barani ulaya .
Familia ya Malkia Elizabeth ambayo inafahamika kama familia ya Windsors yenyewe ina utajiri wa paundi milioni 295 ikiwa inaongoza mataifa ya Uingereza na visiwa vyake vinne , Canada , Australia , New Zealand na maeneo mengine ya jumuiya ya madola .
Malikia Elizabeth na familia yake wana utajiri wa paundi milioni 295.
Utajiri wa familia hii ya kfialme ya Uholanzi unadhaniwa kuwa mkubwa zaidi ya makadirio haya kutokana na ukweli kuwa haujawahi kutamka wazi kiasi cha fedha kinachomilikiwa na familia hii .
Familia ya Bernadotte ya Sweden ambayo inaongozwa na Mfalme Carl Gustaf XVI inashika nafasi ya tano nyuma ya familia inayoongoza Uholanzi .
Familia
ya kifalme ya Hispania ni moja kati ya familia zenye utajiri mdogo japo
inamiliki kasri kubwa kuliko zote za kifalme duniani .
Mfalme wa Norway Harald V ndiye kiongozi mwenye utajiri kiduchu kuliko wote akiwa na kiasi cha Paundi milioni 12 pekee
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI
Post a Comment