Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati, Maji na Mafuta (Ewura), Felix
Ngamlagosi (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari
ofisini kwake Dar es Salaam leo, kuhusu mwenendo wa bei za mafuta nchini
na katika soko la Dunia. Kulia ni Mkurugenzi wa Petroli, Godwin Samwel.
Mkurugenzi wa Petroli, Godwin Samwel (kulia), akizungumza katika mkutano huo.
Ofisa Mawasiliano wa Ewura, Titus Kaguo (kushoto), akizungumza katika mkutano huo.
Wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo.
MAMLAKA ya Udhibiti wa Nishati, Maji na Mafuta
(Ewura), imepunguza bei za mafuta kote nchini kuanzia leo kutokana na
kudorora kwa uchumi wa bara la ulaya.
Hayo yalibainishwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa
Nishati, Maji na Mafuta (Ewura), Felix Ngamlagosi wakati akizungumza na
waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam leo mchana, kuhusu
mwenendo wa bei za mafuta nchini na katika soko la Dunia.
Alisema kuanzia leo bei ya mafuta ya petroli kwa lita moja itauzwa
sh.1955 na hiyo inatokana na kushuka kwa jumla ya asilimia 16 sawa na
pungufu kwa jumla ya sh.311 kwa lita.
Alisema bei ya petroli katika soko la dunia imeshuka kwa jumla ya
aasilimia 25 kuanzia Julai hadi Novemba 2014, sawa na pungufu kwa jumla
ya dila 249 kwa tani.
Ngamlagosi alisema mafuta ya dizeli kwa lita moja yatauzwa sh.1846
na kuwa bei hiyo imeshuka kwa asilimia 13 sawa na pungufu kwa jumla ya
sh.244 kwa lita na kuwa dizeli kwa soko la dunia imeshuka kwa jumla ya
asilimia 28 kuanzia Julai hadi Novemba 2014 sawa na pungufu kwa jumla ya
dola 189 kwa tani na kuwa mafuta ya taa yatauzwa sh. sh.1833 kwa lita.
Alisema katika kipindi cha robo ya mwisho wa mwaka kuanzia mwezi
Septemba hadi Desemba 2014, bei za mafuta ghafi zimekuwa zikishuka kwa
kasi ikilinganishwa na kipindi cha hapo nyuma ambapo zimeshuka toka dola
100 kwa pipa hadi kufikia wastani wa dola 60 kwa pipa moja ambayo ni
sawa na karibu asilimia 40.
Alisema viwango hivyo vya bei iliyopungua ni katika soko la Dar es
Salaam na mikoa mingine bei zao zimepangwa kutokana na kuwepo kwa
gharama za usafirishaji.
Ngamlagosi alitoa mwito kwa wanunuaji wa mafuta hayo kuhakikisha
wanapatiwa lisiti baada ya kununua kwani itasaidia kuwabaini
wafanyabiashara wasio waaminifu ambao wataendelea kuuza kwa bei ya
zamani.
"Natioa mwito wa kuwaomba wanunuaji wa mafuta kuhakikisha wanapewa
lisiti kwani itatusaidia kuwabaini wale wanauza kwa bei ya juu, na pia
itamsaidia mnunuzi iwapo atauziwa mafuta yaliyochini ya kiwango na
ukusanyaji wa kodi ya serikali" alisema Ngamlagosi.
Naye Mkurugenzi wa Petroli, Edwin Samwel alisema Ewura imejipanga
vizuri kuhakikishha hakuna ujanja ujanja utakaojitokeza wa kudai mafuta
yamekwisha au yaliyopo yatauzwa kwa bei yaliyonunuliwa.
Alisema mfanyabiashara yeyote atakayekiuka utaratibu huo
atachukuliwa sheria pamoja na kufungiwa biashara yake ingawa alisema
hali hiyo haitajitokeza.
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI.
Post a Comment