Davina alifunguka hayo juzikati katika mahojiano maalumu na paparazi wetu ambapo alisema mwaka huu unakuja kukiwa na changamoto nyingi kutokana na matukio mbalimbali yanayoendelea kutokea hivyo viongozi na Watanzania kwa ujumla wanatakiwa kuwa makini ili kuepuka umwagaji wa damu.
“Huu mwaka mzito sana na tunaweza kufurahi lakini kumbe kuna baadhi ya viongozi wanapanga kufanya mambo ya ajabu, tumeona uchanguzi wa Serikali za Mitaa juzi mambo yalivyokuwa, viongozi na Watanzania wenzangu lazima tuwe macho na sisi wapiga kura tumpinge kiongozi yeyote atakayetaka madaraka kwa njia ya vurugu,” alisema Davina.
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI.
Post a Comment