MSANII wa filamu Bongo, Tamrina Poshi maarufu kama
Amanda, amechafuka baada ya mtu anayejitambulisha kwa jina lake,
kujinadi kwa kujitongozesha katika mtandao wa kijamii wa Facebook.
Msanii wa filamu Bongo, Tamrina Poshi maarufu kama 'Amanda'.
Amanda huyo feki amekuwa akijiuza bila aibu katika mtandao huo kwa
kujitongozesha kwa wanaume, kitu kinachomuumiza muigizaji huyo ambaye
pia anawashangaza wasanii wenzake juu ya tabia hiyo ya kuchefua.
“Yaani nimekuwa nikiulizwa sana, lakini juzi ndipo nilishtuliwa na
msanii mwenzangu, nikafanya uchunguzi na kugundua kwamba kuna mtu
ananichafua kupitia mtandao, mashabiki wangu watambue kuwa mimi sijawahi
kujiuza na ninajiheshimu,” alisema Amanda.
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI
Get Free Email Updates to your Inbox!
Post a Comment