Msanii wa filamu Bongo, Tamrina Posh ‘Amanda’ amesema mwaka uliopita wa
2014 ulikuwa mbaya sana kwake kwani aliandamwa na majanga yaliyotikisa
maisha yake.
Msanii wa filamu Bongo, Tamrina Posh ‘Amanda’.
Akizungumzia namna alivyoupkea mwaka wa 2015 Amanda alisema, kwanza
anamshukuru Mungu kwa kuuona akiwa mzima lakini akamuomba amuepushe na
mabalaa kwani uliopita haukuwa rafiki kwake.
“Mwaka 2014 bora umeisha, ulikuwa mbaya sana kwangu, mwanzo ulikuja
vizuri lakini nikashangaa katikati ukanigeuka, nimenusurika kifo lakini
namshukuru Mungu naendelea kupumua hadi leo,” alisema Amanda.
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI.
Get Free Email Updates to your Inbox!
Post a Comment