Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

Wasanii 10 waliotikisa katika filamu 2014

NIKIWA kama mpenzi wa filamu za kibongo Tanzania ninakuletea orodha ya waigizaji 10 waliofanya vizuri mwaka 2014.
Naamini kwa yule mpenzi wa kuangalia filamu hata pingana na mimi kwa hiki nilichokiandika kutokana na kujua juhudi za wasanii hawa katika msimu wa 2014.
Jacob Stephen aka 'JB'
Mwaka huu, mmiliki wa Jerusalem Films na mwongozaji wa filamu nyingi zinazozalishwa na kampuni hiyo, JB ametamba na filamu kama ‘Hukumu ya Ndoa’ na ‘Mikono Salama’ambazo aliziongoza pia. Filamu nyingine alizoziongoza ni pamoja ‘Wageni Wangu’ pamoja na ‘Chausiku’.
Salim Ahmed 'Gabo'
Hakika msanii huyu msimu huu ameonesha uwezo wakutosha kutokana na kujua nini anakifanya katika tasnia ya filamu kwa kuigiza kwa kubeba uhusika.
Mwaka jana msanii huyu alitamba na filamu ya ‘Bado Natafuta’ ambayo bado inaendelea kufanya vizuri sokoni. Mwaka huu Gabo pia ameonekana kwenye filamu nyingi ikiwemo ‘Siri Ya Giningi’ iliyofanya vizuri sokoni akishirikiana na Sabby Angel pamoja na Mzee Korongo.
 Kinachomfanya mwigizaji huyu apendwe ni ule uwezo wake wa kubeba uhusika.
Shamsa Ford
Mwaka jana Shamsa  alifanya vema kwa filamu ya Bado Natafuta akiwa na Gabo. Mwaka huu ameweza kutikisa tena kwa mauzo ya filamu yake ya Chausiku inayodaiwa kufikia rekodi ya mauzo iliyowekwa na marehemu Steven Kanumba kupitia filamu yake ya mwisho, Ndoa Yangu.
Amesema anatamani mafanikio makubwa zaidi katika mwaka ujao kuliko aliyoyapata ndani ya 2014 hasa kupitia kazi yake ya 'Chausiku'.
Salma Jabu 'Nisha'

Nisha ambaye amewahi kutamba na filamu kama Tikisa, Pusi na Paku mwaka huu mwanadada huyo aliachia filamu ya komedi, Zena na Betina inayofanya vizuri sokoni.
Jacqueline Wolper
Pamoja na hivi karibuni kuviambia vyombo mbalimbali vya redio kuwa bado yupo benchi kucheza filamu zake binafsi kutokana na mapato kuwa finyu, mwaka huu alitoka na filamu ya Tom Boy. Pia ameonekana kwenye filamu ya VIP iliyoingia sokoni Oktoba.

Irene Uwoya 'Uwoya'
Mwaka huu Irene ameonekana kwenye filamu kama Jamal na Nesi Bandia ambazo zote zimefanya vizuri sokoni.

King Majuto 'Mzee Majuto'
 
Mzee Majuto anaendelea kufanya vizuri sokoni kutokana na filamu kama Duplicate, Chungu Kimoja, Nahama na zingine.


Vincent Kigosi 'Ray'
Ray kupitia kampuni yake, RJ Company ameendelea kufanya vizuri na hivi karibuni aliachia filamu ya VIP akiwa na Wolper Salha na wengine.

Issa Mussa  'Cloud'
Cloud ameendelea kufanya filamu zenye visa vya kuvutia kama Fundi Selemala na Doctor Max zilizotoka mwaka huu.

Ringo na Tin White
Hii ni timu ya watu wawili. Wasanii hawa wa vichekesho wanapendwa sana na hata kazi zao zinapoingia sokoni huuza.
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI.

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright BONGO HABARI
Back To Top