Tume ya Taifa ya Uchaguzi imetoa ufafanuzi kuhusu ushiriki wa Wanajeshi katika uboreshaji wa zoezi la uandikishaji wa daftari la kupiga kura.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Tume inasema kutakuwepo na wanajeshi 6 wa Jeshi la Wananchi katika kila kituo ambao kazi yao ni kusaidia shughuli za lojistiki kama vile kuhamisha vifaa kutoka kata moja kwenda nyingine.
Pia wanajeshi hao watasaidia katika shughuli za kufanya matengenezo madogo madogo ya vifaa yanayoweza kujitokeza wakati wa zoezi la uandikishaji.
Taarifa inasisitiza kuwa Wanajeshi hao hawatakuwepo kwenye vituo vya uboreshaji wala hawatahusika na zoezi la uandikishaji kama baadhi ya vyombo vya habari vilivyoripoiti hivi karibuni.
Aidha katika mkutano na Vyama vya Siasa uliofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam ulifafanua kuwa watendaji watakaohusika katika zoezi hilo ni maafisa waandikishaji na wasaidizi wao, waandishi wasaidizi, wataalamu wa fani ya TEHAMA na wataalamu kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI.
Post a Comment