Msanii wa filamu Bongo, Shamsa Ford.
Ni wiki nyingine tena mpenzi msomaji tunakutana katika safu hii ya
maswali kumi na leo tunakuletea msanii wa filamu Bongo, Shamsa Ford
ambaye alibanwa kwa maswali na mwandishi wetu Gladness Mallya.Ijumaa: Ni muda mrefu tangu tuliposikia habari za uchumba wako na Dickson, mbona mambo ya ndoa kimya?
Shamsa: Kwa wasiojua ni kwamba, tulishafunga ndoa ya kimila, ile ya kanisani ndiyo bado, tunasubiri siku ambayo Mungu ametupangia.
Ijumaa: Inasemekana kwa yule bwana wako umekufa na umeoza, yaani anampenda kuliko maelezo, sababu hasa ni ipi?
Shamsa: Unajua tena moyo ukipenda ila pia niliona ananifaa katika maisha yangu kwani ana imani, busara, hekima pia ana hofu ya Mungu.
Ijumaa: Wewe ni msichana mzuri, unajiepusha vipi na vishawishi vya wanaume wakware ambao hutumia pesa na mali zao kurubuni wanawake?
Shamsa: Ushawishi upo na wanaochukuliwa
kirahisi ni wale wasiojitambua. Mimi najitambua ni nani katika jamii
hivyo si rahisi kuingia kwenye mitego ya wanaume hao.
Ijumaa: Inasemekana Bongo Muvi kwa kuchukuliana mabwana hamjambo, vipi siku ukisikia yule mchumba wako anatoka na shosti wako?
Ijumaa: Inasemekana Bongo Muvi kwa kuchukuliana mabwana hamjambo, vipi siku ukisikia yule mchumba wako anatoka na shosti wako?
Shamsa Ford.
Shamsa: Ni jambo ambalo silifikirii kwa kuwa mume wangu namuamini sana. Ijumaa: Kuna tetesi kwamba huwa unatumia dawa za Kichina kukuza makalio na matiti na ndiyo maana kadiri siku zinavyokwenda unazidi kufutuka, hili likoje?
Shamsa: (Anacheka) Sijawahi kutumia dawa yoyote katika mwili wangu na hata ukiniangalia sasa hivi na miaka mitatu iliyopita nyuma sina mabadiliko makubwa kivile.
Ijumaa: Hivi leo hii usingekuwa unauza nyago kwenye filamu ungekuwa unafanya kazi gani?
Shamsa: Nadhani ningekuwa mfanyabiashara kwani ni kazi ninayoimudu pia.
Ijumaa: Taarifa zilizopo ni kwamba, wewe na Welu Sengo ni paka na chui kiasi kwamba bifu lenu linatishia amani, hili nalo vipi?
Shamsa: Mh! Kwa kifupi mimi sina bifu na msanii yoyote, hayo ni maneno ya watu tu.
Ijumaa: Inadaiwa wewe ni msichana unayejidai na kujisikia kiasi kwamba huna mashosti, ni kwa nini?
Shamsa: Mara nyingi mimi nakuwa bize na kazi zangu, pia sipendi kuwa na marafiki kwa sababu sitaki kugombana na watu maana kwenye makundi ya mashosti kuna ugomvi sana.
Ijumaa: Kwa staili hii ya mabifu kati ya wasanii wa Bongo Muvi unadhani sanaa itapiga hatua inayotakiwa?
Shamsa: Mimi nachukia sana mabifu kwa kuwa najua hayana faida. Waswahili wanasema umoja ni nguvu, tukiwa hatupendani ni dhahiri hatuwezi kufanikiwa.
Ijumaa: Mwaka 2014 ndiyo huo unaelekea ukingoni, je ulikuwaje kwako?
Shamsa: Mwaka huu unaisha vizuri sana kwangu kwani nilimuomba Mungu nifanye kazi itakayokubalika katika jamii na kweli alinifanikisha kufanya filamu ya Chausiku na imefanya vizuri hivyo namuomba anisaidie na huo unaokuja mambo yaende vizuri.
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI.
Post a Comment