Kulikuwa na maongezi yakiendelea ambapo
viongozi mbalimbali wa Afrika hawakupendezwa na kitendo cha Rais wa
Kenya, Uhuru Kenyatta kufunguliwa mashtaka kwenye Mahakama ya ICC huku
mjadala wa viongozi hao ikiwa ni kujitoa kwenye Mahakama hiyo.
Kama ulipitwa na story hiyo, hapa kuna
kile kilichozungumzwa na Rais wa Uganda, Yoweri Museveni kuhusu msimamo
wake na Mahakama ya ICC.
“… Nitaleta motion
kwa African Union kikao kijacho.. Nataka sisi wote tutoke kwenye Court
hiyo ya wazungu wakae na Court yao… Hiyo Court niliunga mkono mwanzoni
kwa sababu mimi ni mtu ambaye napenda nidhamu, sitaki watu kufanya
madhambi bila kuwajibika.. Lakini wameifanya chombo cha kukandamiza
Afrika jela kwa hiyo nimemalizana na hiyo court… Sitafanya kazi nao
tena…”– Rais Museveni.
Hapa kuna video niliyoitoa Citizen TV ambapo unaweza kusikiliza na kutazama taarifa hiyo kwa ukamilifu.
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI.
Post a Comment