Sosi wa habari hii alisema kuwa Paka yule alikuwa eneo la Methadone Mwananyamala Hospitali ambapo mwanamuziki huyo anakunywa dawa.
Staa anayetamba na ngoma mpya ya ‘Nshumu nshumu’, Rehema Chalamila ‘Ray C’.
“Alipopita Ray C alirukiwa na paka na kumgangania mguu alijaribu
kumzuia lakini hakufanikiwa kitendo kilichozua utata kwani bila watu
kumsaidia paka yule asingetoka mguuni kwake”, alisema Sosi.Aidha Sosi huyo alisema kuwa baada ya paka huyo kumvamia mambo yake yamekuwa magumu ni mtu ambaye anaomba hata mia tano na kwa sasa amefunga mghahawa wake.
“ Yaani Ray C kwa sasa anatia aibu kwani maisha yamemharibikia mpaka watu wanadai kuwa huenda yule paka hakuwa wa heri, amekuwa mlevi anavuta sigara ovyo mpaka mwenye nyumba wake hamtaki tena nadhani mkataba wake umesitishwa”, alisema Sosi.
Baada ya habari hizi kutua kwenye meza ya Ijumaa mwandishi alimwendea hewani Ray C ambaye alikiri kuvamiwa na paka na kudai kuwa yeye haamini kama unaweza kuwa ni uchawi anahisi alimkanyaga mkia bila kujua.
“Yaani watu wanapenda kuongea sana mimi kwa sasa mambo yangu yanaenda vizuri tu si mnaona hata nyimbo nimetoa, paka ni sihu ya siku nyingi mpaka nishapona jeraha, duka nimefunga kwasababu nataka kufungua duka kubwa la nguo na nusu yake nitafungua ofisi nyingine, ” alisema Ray C Aidha Ray C alipinga vikali suala la kuvuta sigara na kudai kuwa watu wanaompakazia wana nia ya kumharibia mambo yake kwasababu kwa sasa wameona ana maendeleo.
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI.
Post a Comment