Klabu ya Manchester City imezindua kituo chake cha kisasa ambacho kimegharimu paundi milioni 200 karibu na ulipo uwanja wake wa nyumbani wa Etihad.
Kituo hicho cha kisasa kina viwanja kadhaa vya nje na ndani huku kukiwa na sehemu kadhaa za kufanyia mazoezi kwa timu ya kwanza na timu za vijana .
Kituo hicho kina lengo la la kuhakikisha kuwa Manchester City inaondokana na utamadunia wa kununua wachezaji kwa bei ghali na badala yake kutengeneza nyota wake wenyewe ambao watakuwa wanaendelezwa kwenye kituo hicho .
Kituo hicho ambacho kimechukua miaka sita kujengwa kinafahamika kama City Football Academy na kimegharimu jumla ya paundi milioni 200 ambazo zimewekezwa na mmiliki wa klabu hiyo anayefahamika kama Sheikh Mansour .
Kituo hiki kinatimiza ahadi ambayo Sheikh Maosur aliiweka wakati alipoinunua Manchester City mwaka 2008 ambapo aliahidi kuwa atahakikisha anaijenga klabu hiyo na kuifanya kuwa klabu ya kisasa inayokwenda na wakati na si kuwa na kawaida ya kununua wachezaji nyota pekee.
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI.
Post a Comment