Taarifa za usajili na kuachwa wachezaji zinazidi kuingia na safari hii inasemekana kuwa kiungo Mbrazil Emerson amekuwa mhanga wa kwanza wa kuondoka kwa kocha Mbrazil Marcio Maximo baada ya mchezaji huyo kuachwa na Yanga.
Mbrazil huyo anaondoka Yanga baada ya kucheza mechi moja pekee dhidi ya Simba ambako Yanga ilifungwa 2-0.
Emerson alishindwa kuwaridhisha
mashabiki wa Yanga ambao wengi walionyesha kukerwa na uwezo mdogo wa
kiungo huyo katika dakika 45 alizocheza kwenye mechi dhidi ya Simba.
Emerson alikuja nchini siku chache
zilizopita ambapo alipaswa kuziba nafasi iliyoachwa wazi na mshambuliaji
Genilson Santos Santana Jaja ambaye hakurudi baada ya kuondoka nchini
kufuatia kusimama kwa ligi.
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI.
Post a Comment