Katika hali ya kawaida namba zinazoandikwa kwenye jezi za wachezaji wa timu za mchezo wa soka huwakilisha nafasi wanazocheza uwanjani .
Namba hizi kiasili huendana na eneo ambalo mchezaji husika anapendelea kucheza kwa mfano jezi namba moja huvaliwa na kipa , jezi namba tisa huvaliwa na mshambuliaji na kadhalika na kadhalika .
Utamaduni huu umekuja kubadilika hivi karibuni ambapo Wachezaji wamekuwa na kawaida ya kuvaa jezi kutokana na ukaribu walio nao na mnamba Fulani au wakati mwingine sababu za kihistoria na mazoea pia yamekuwa yakiongoza utamaduni wa kuvaa namba husika .
Mshambuliaji
wa Ivory Coast Wilfred Bony ni moja kati ya wachezaji wanaovaa jezi
namba 10 wanaofanya vizuri kwenye ligi ya England .
Hili limeweza kudhihirika msimu huu kwenye ligi ya England ambako wachezaji wanaovaa jezi namba 10 wameongoza kwa kung’aa hasa kwenye ufungaji wa mabao muhimu .
Takwimu zinaonyesha kuwa kati ya mabao 457 ambayo yamefungwa hadi sasa kwenye mechi za ligi kuu ya England mabao 56 yamefungwa na wachezaji wanaovalia jezi hii ambayo siku zote inahusishwa na ‘mafundi’ wa mpira .
Romelu Lukaku ni mchezaji mwingine anayevaa jezi namba 10 .
Katika kundi la wachezaji wanaovaa namba 10 wako nyota kama Eden Hazard , Wayne Rooney , Wilfred Bony , Jack Wilshere na Romelu Lukaku huku Bony na Rooney wakiongoza orodha hiyo wakiwa wamefunga mabao 8 .
Wafungaji Bora kuendana na namba za Jezi
Namba Idadi Ya Magoli
1. Na 10 – 56
2. Na 9 – 38
3. Na 18 – 33
4. Na 19 – 32
5. Na 23 – 24
6. Na 11 – 23
6. Na 16 – 23
6. Na 17 – 23
7. Na 15 – 22
8. Na 21 – 19
*Takwimu hizi ni kwa msimu huu pekee.
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI.
Post a Comment