Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

First Eleven ya Pluijm Yanga SC hii hapa

 
Dunny Mrwanda.
AKIWA na siku nne za kuifundisha timu hiyo, Kocha Mkuu wa Yanga, Mholanzi, Hans van Der Pluijm tayari amepata kikosi cha kwanza atakachoanza nacho kuivaa Azam FC.Timu hizo, zinatarajiwa kuvaana katika mechi ya Ligi Kuu Bara, itakayopigwa Desemba 28, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini, Dar es Salaam.
Pluijm alianza kibarua cha kukinoa kikosi hicho Jumamosi ya wikiendi iliyopita mara baada ya aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo Mbrazili, Marcio Maximo kutimuliwa.Katika mazoezi yake hayo ya siku nne, kocha huyo alionekana akikiandaa kikosi hicho kwa kuwapanga pamoja na kuwapa mbinu mbalimbali za ndani ya uwanja kuanzia mabeki, viungo na washambuliaji.
Kocha huyo, katika kikosi hicho cha kwanza kinatarajiwa kuwa na sura mpya nne zitakazoanza kuonekana kwenye mechi dhidi ya Azam FC, ambazo ni Salum Telela aliyekuwa anaanzia benchi, Danny Mrwanda, Amissi Tambwe na Kpah Sherman waliotua kuichezea timu hiyo katika usajili wa dirisha dogo.
Wakati hawa wanaingia Andrey Coutinho, Jaja ambaye ameshatimka, Hassan Dilunga na  Juma Abdul ambao walikuwa na nafasi ya kuanza kwenye mechi nyingi kipindi cha Maximo hawapo kwenye kikosi hiki cha Pluijm.
Andrey Coutinho.
Kikosi hicho cha kwanza kinatarajiwa kuundwa na Deogratius Munishi ‘Dida’, Mbuyu Twite, Oscar Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kelvin Yondani, Salum Telela, Mrisho Ngassa, Haruna Niyonzima, Tambwe, Sherman na Mrwanda.
Wakati kikosi hicho kikiandaliwa, kwenye mechi ya Azam FC huenda kukawepo na mabadiliko kidogo kutokana na Cannavaro kutumikia adhabu ya kadi nyekundu aliyoipata wakati timu yake ilipocheza na Kagera Sugar.
Hivyo, kutokana na Cannavaro kutumikia adhabu hiyo, nafasi yake inatarajiwa kuchukuliwa na Twite atakayecheza pamoja na Yondani huku Telela akicheza namba mbili huku Saidi Juma akicheza namba sita ya Twite.
“Baada ya siku tano nitakuwa nimeshajua kabisa nani atakuwa wapi na nani wapi nimeanza kazi hivi karibuni sidhani kama mnatakiwa kuwa hofu sana,” alisema Pluijm.Yanga inashika nafasi ya pili kwenye ligi kuu ikiwa na pointi 13, baada ya kucheza michezo saba, ushindi hapa unamaana kuwa Yanga watafikisha pointi 16 ambazo ni moja zaidi ya kinara Mtibwa Sugar.
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI.

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright BONGO HABARI
Back To Top