Pazia la mechi za ligi kuu ya England katika ‘Boxing Day’ limefungwa kwa mchezo wa ‘London Derby’ kati ya Arsenal dhidi ya Queens Park Rangers.
Wakiwa wametoka kupata sare ngumu ya 2-2 dhidi ya Liverpool wiki iliyopita, Gunners leo wamefanikiwa kuingia kwenye sita bora ya Barclays Premier League baada ya kushinda dhidi ya vijana wa Harry Redknapp.
Alexis Sanchez ambaye kwenye mchezo huo alikosa penati katika dakika za mwanzo za kipindi cha kwanza, alisahihisha makosa yake kabla ya kipindi cha kwanza hakijaisha kwa kuipa Arsenal goli la kusawazisha.
Kipindi cha pili kilianza kwa Gunners kupata upungufu uwanjani baada ya Oliver Giroud kupewa kadi nyekundu kwa kumpiga kichwa Onouah wa QPR.
Kadi nyekundu haikupunguza nguvu ya Arsenal mapema na muda mfupi baadae Thomas Rosicky alifanikiwa kuipa timu yake goli lake la pili.
Katika dakika za mwisho QPR walicharuka kutaka kusawazisha lakini waliishia kupata goli moja tu kwa mkwaju wa penati kupitia Charlie Austin – lakini mchezo unamalizika Arsenal 2-1 QPR.
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI.
Post a Comment