Chama
Cha Mapinduzi (CCM) kinaingia katika uchaguzi wa serikali za mitaa
kesho, kikiwa kimeshajizolea maelfu ya nafasi ambazo wagombea wake
wamepita bila kupingwa.
Akihutubia kwenye mkutano wa kufunga kampeni za uchaguzi huo, katika Mtaa wa Mtambani B, Kata ya Jangwani, jimbo la Ilala jijini Dar es Salaam, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye alisema, kulingana na takwimu CCM imepita bila kupingwa katika vijiji 2708, mitaa 644, na vitongoji zaidi ya 26,300.

Alisema,
CCM imeweza kupita bila kupigwa baada ya vyama vya upinzani kushindwa
kusimamisha kabisa wagombea na maeneo mengine kuweka wagombea ambao
walionekana kukosa sifa za kugombea baada ya kuwekewa pingamizi.
Nape
alisema, hatua hiyo ya CCM kuingia kwenye uchaguzi huo ikiwa na mtaji
mkubwa wa nafasi ambazo wagombea wake amepita bila kupingwa ni dalili
tosha kwamba chama kitavibwaga vibaya vyama vya upinzani kuliko uchaguzi
uliopita mwaka 2009.
"Uchaguzi
uliopita wa serikali za mitaa CCM iliibuka na ushindi wa asilimia 96,
sasa kutokana na dalili za mapema, uchaguzi wa safari hii sina shaka
kabisa kwamba wapinzani tutawapiga kwa ushindi wa asilimia mia moja",
alisema Nape.
Nape
aliupongeza uongozi wa CCM katika jimbo la Ilala, baada ya
kumthibitibishia kwamba katika kipindi chote cha kampeni jimbo hilo
wamekuwa wakifanya kampeni za kistaarabu na wanao uhakika wa kuibuka na
ushindi kwa asilimia mia moja baada ya uchaguzi.
"Sina shaka kabisa kwamba hapa Ilala tutashinda kwa kishindo, mnastahili kupata pongezi kutoka makao makuu kutokana na mlivyoendesha kampeni, hongereni sana.". alisema Nape.
"Sina shaka kabisa kwamba hapa Ilala tutashinda kwa kishindo, mnastahili kupata pongezi kutoka makao makuu kutokana na mlivyoendesha kampeni, hongereni sana.". alisema Nape.
Alisema,
pamoja na CCM kuwa na uhakika wa kushinda lakini itafanya kazi ya ziada
ya kuhakikisha wapigakura waliojiandikisha wanapata fursa ya kwenda
kupiga kura bila kubughudhiwa na watu ambao huandaliwa na vyama vya
upinzani kufanya fujo ili kuzuia watu wasijitokeze kupiga kura.
"Vijana
wa CCM lazima tuwe shupavu, maana kujifanya wanyonge unyonge huu
hautatusaidia chochote, na hili mimi sihamasishi fujo na si wa kwanza
kulisema hata Mwenyekiti wetu wa CCM alishasema kwamba unyonge basi.
Sasa mimi hapa napigilia msumari tu".
Nape
aliwataka wananchi wa Ilala na Watanzania kwa jumla kuchagua wagombea
wa CCM, kwa kuwa ana uhakika ndio watakao watumikia vizuri.
Aliwataka
viongozi watakaochaguliwa katika uchaguzi huo wa serikali za mitaa
kuhakikisha wanawatumikia wananchi, hasa kwa kusimamia kuondoa kero zao
na kusimamia misingi ya kuboresha mazingira ya shughuli mbalimbali
zikiwemo za biashara kama za mamalishe na machinga.
Nape alisema, CCM, itaendelea kusimamia na kutetea haki za wananchi hasa walio wanyonge na si kwa sababu ya kutaka kura ila kwa sababu ni wajibu wake kama chama kilichopewa ridhaa ya kutawala nchi.
Nape alisema, CCM, itaendelea kusimamia na kutetea haki za wananchi hasa walio wanyonge na si kwa sababu ya kutaka kura ila kwa sababu ni wajibu wake kama chama kilichopewa ridhaa ya kutawala nchi.
Katika
mkutano huo, Nape aliwanadi wagombea wa nafasi mbalimbali katika Mtaa
huo wa Mtambani B, akiwemo mgombea wa nafsi ya Ueneyekiti wa mtaa huo,
Gungu Tambaza
Katibu
wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisalimiana na baadhi ya
viongozi wa CCM baada ya kuwasili katika mkutano wa kufunga kampeni za
Uchaguzi wa serikali za Mitaa za Jimbo la Ilala, Dar es Salaam, jana
jioni
Wana CCM wakimshangilia Nape alipowasili kwenye mkutano huo
Wananchi wakimshangilia Nape alipowasili kwenye mkutano huo
Nape akiwa Jukwaa Kuu pamoja na viongozi wa CCM baada ya kuwasili kwenye mkutano huo
Lwiza Mbutu akiongoza bendi ya Twanga Pepeta kutumbuiza baada ya kuwasili Nape kwe ye mkutano huo.
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI.
Post a Comment