Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

WEMA, PENNY WAPATANA

 
HATIMAYE mastaa wawili wakubwa Bongo, Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu na Mtangazaji wa Redio EFM, Peniel Mungilwa ‘Penny’ wamepatana baada ya kuwa katika bifu kwa kipindi kirefu, chanzo kikiwa ni penzi la Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’.

 
Wema Sepetu akiwa na shosti yake Peniel Mungilwa ‘Penny’.
Habari za ndani zinaeleza kuwa wawili hao walipatanishwa na mdau mkubwa wa burudani, Jennifer Pemba kwenye sherehe ya siku yake ya kuzaliwa iliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita katika Ukumbi wa East 24 Bar and Grill uliopo ndani ya Hoteli ya Sea Cliff, Masaki jijini Dar es Salaam ambapo wawili hao walialikwa.
Tukio hilo la kupatana linakuja siku chache baada ya Wema kummwaga aliyekuwa laaziz wake, Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ ambaye pia amewahi kutoka kimapenzi na Penny.
Mtangazaji wa Redio EFM, Peniel Mungilwa ‘Penny’.
“Ilikuwa kazi kuwafanya wapatane, lakini Jennifer alifanya juhudi kubwa kwa kuzungumza nao, si unajua zamani walikuwa paka na panya?“Uhasama wao ulitokana na kitendo cha Penny kumchukua Diamond wakati wao wakiwa ni marafiki wakubwa, hilo likamkera sana Wema,” kilisema chanzo chetu na kuanza bifu rasmi na Penny.
Kwa mujibu wa chanzo hicho, Penny amefurahishwa na kitendo cha Wema kummwaga Diamond  na ameahidi  kuanzia sasa atakuwa Team Wema mwanzo mwisho.
 
Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu.
Wawili hao walipotafutwa juzi kwa njia ya simu ili kuzungumzia kupatana kwao, hakuna aliyekuwa hewani huku chanzo kikisema walichelewa kwenye sherehe huenda muda waliotafutwa walikuwa bado wamelala.
Picha zinazoonekana kwenye habari hii ni muda muda mfupi baada ya kupatana. Kwa habari zaidi endelea kufuatilia Magazeti ya Global Publishers.

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright BONGO HABARI
Back To Top