
Polisi
wa kutuliza ghasia, wakifanya doria kwenye mitaa ya jiji la Mwanza
baada ya kutokea ghasia kufuatia askari wa jiji hilo kufanya jaribio la
kuwaondoa wamachinga kwenye soko kuu, rwagasore na mtaa wa Lumumba
mapema leo Jumatano Novemba 19, 2014

Polisi
wa kutuliza ghasia wakiwa wamejihami kwa silaha wakati wakituliza
ghasia za wamachinga kwenye mitaa ya jiji hilo mapema leo Jumatano
Novemba 19, 2014. Zogo hilo lilizuka baada ya askari wa jiji
walipowavamia wamachinga na kuwaamuru waondoke
kwenye maeneo ya soko kuu,
Rwagasore na mtaa wa Lumumba na hapo ndipo "Kasheshe" lilipozuka ambapo
askari wa jiji walizidiwa nguvu kutokana na mawe yaliyokuwa yakirushwa
na wamachinga mithili ya maroketi na kuwafanya warudi nhyuma na ndipo
polisi wa kutuliza ghasia walipoitwa na kuwakabili wamachinga hao.

Moja
ya barabara za jiji la Mwanza ikionekana kuwa nyeupe huku watu wachache
wakitafuta mahala salama baada ya polisi kupambana na wamachinga mapema
leo Jumatano Novemba 19, 2014

Machinga,
akirusha jiwe, wakati polisi wa kutuliza ghasia walipoingia mtaani na
kupambana na wafanyabiashara ndogondogo jijini Mwanza maarufu kama
wamachinga, leo Jumatano Novemba 19, 2014
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI.
Post a Comment