Kwa mujibu wa msemaji wa kanisa hilo, Kuhani, Kiongozi Miaka 1,000 aliwaambia kuwa amekamilisha kujenga msingi wa kanisa la mwisho la kizazi cha nne.
Alifafanua kwamba, baada ya miaka 1,000 ya kanisa, walianza mwaka wa kwanza ambapo alitambulisha tarehe ya Kimungu (Kirumi) kwa maana hiyo yeye alifanya kazi ya utumishi kwa miaka 12 na hatimaye aliikamilisha.
“Alifanya kazi kwa muda wa miaka 12 hadi anatwaliwa lakini kwa kawaida hatuna mwaka wa kumi na ukiangalia miaka yetu tunaanza na 1-9, halafu tunaanza tena na moja hivyo nabii wetu alikuwa kwenye uongozi kwa mwaka wa tatu kabla hajatwaliwa na Mungu,” alisema Kuhani.
Lango kuu la kanisa hilo.
Miongoni mwa kile kinachozungumzwa juu ya tukio hilo na kuacha
viulizo kwa makuhani hao ni baada ya kuwaambia kuwa, gari lake lilikuwa
linakuja kumchukua mchana wa siku hiyo bila wao kuelewa alichokuwa
akimaanisha kwa ufasaha.“Hili liliacha viulizo sana kwa sababu gari lake alimaanisha kuwa ndicho kifo chake na katika miujiza kweli akafa mchana huo.
“Kusema kweli hili kanisa lina bahati sana. Elia tulikuwa naye hapa japokuwa amekwenda, lakini tumebaki naye kiroho. Tunaamini atarudi kama Yesu,” alisema kuhani huyo.
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI.
Post a Comment