
Anasema kuwa,hatopenda kuchanganya mambo yake ya familia na biashara ya muziki hivyo anatarajia kupata mtoto na kuolewa mara baada ya kumaliza albamu yake Tano. Mkali huyo wa muziki wa kufoka foka nick Minaji anasema kuwa atakapokuwa na mtoto, atatumia muda mwingi kuwa nae, na hatopenda kuona watoto wake wahisi kama hawapi matunzo kwa umakini hivyo anatarajia kupumzika muziki kwa muda.

Msanii huyo kutoka familia ya Young Money anasema kuwa endapo atamaliza albamu yake ya tano bila kuwa na mtoto itamuhuzinisha kwani anadhani huo ndio muda sahihi kwake kuitwa mama ingawa hatarajii kuzaa kabla ya kuolewa.

Mpaka sasa ana album mbili huku akitarajiwa kutoa albamu ya tatu ThePinkPrint ifikapo mwezi Disemba mwaka huu.
USISITE KUTUACHIA UJUMBE WAKO HAPO CHINI.
Post a Comment