MREMBO Mariam Mohamed
ambaye alishiriki na kushika nafasi ya pili ya Shindano la Miss Mara
mwaka 2003, wiki iliyopita alizusha vurumai kubwa kwa kuzichapa kavukavu
na mumewe usiku baada ya kumkuta akiwa na baamed ndani ya nyumba moja
iliyopo Njiro eneo linalojulikana kama Nguzo Moja jijini Arusha, Amani
lina mkanda kamili.
Mrembo Mariam Mohamed akizichapa kavukavu na mumewe, Rasha Idrisa (38).
Licha ya kuzichapa na mumewe huyo ambaye ni mfanyabiashara aitwaye
Rasha Idrisa (38), mkazi wa Sinza jijini Dar es Salaam, baamed huyo
aitwaye Prisila, naye alipata kipigo kikali toka kwa Miss huyo aliyekuwa
akisaidiana kutoa dozi na mpambe wake.Prissila anayefanya kazi kwenye baa moja iliyopo maeneo ya Njiro (jina linahifadhiwa) alijaribu kujitetea kuwa hakufahamu kama mpenziwe huyo alikuwa mume wa mtu, alishambuliwa sehemu mbalimbali za mwili wake, ikiwa ni pamoja na kukabwa shingo, hali iliyomuacha hoi na kuapa kutoendelea tena kuiba vya watu.
Operesheni Fichuo Maovu (OFM) ya Global
Publishers ilitonywa mapema juu ya kuwepo kwa mpango wa kumfumania
Rasha, anayedaiwa kuwa alisafiri kibiashara akimuaga mkewe kuelekea
Zambia, tokea Agosti mwaka huu.
Mrembo Mariam Mohamed akizidi kumtaiti mumewe.
Chanzo chetu kinadai kuwa kitu kilichompa mashaka Mariam ni wakati
alipokuwa akiwasiliana kwa simu na mumewe, kwani miito yake ilionyesha
kuwa mpigiwaji alikuwa nchini. Baada ya kuona hivyo akaanza udadisi wa
kujua ni wapi hasa alipo mumewe.
Siku chache zilizopita, chanzo hicho
kilisema msichana huyo alipata taarifa kutoka kwa marafiki zake waliopo
Arusha, juu ya kuonekana kwa mumewe akila maisha na msichana mmoja
mhudumu wa baa, na kwamba alikuwa akitanua naye kila siku na mara nyingi
walilala pamoja.
“Mariam amepanga kesho ndiyo aende akawafumanie, kama ni pale baa au wanakoendaga, kwa hiyo nyinyi mnaweza kwenda pale ili mjue kitakachoendelea,” chanzo chetu kiliwasiliana na OFM ambao walifika katika baa anayofanya kazi Prisila bila yeye kufahamu na baadaye Mariam akiwa na mpambe wake nao waliwasili.
“Mariam amepanga kesho ndiyo aende akawafumanie, kama ni pale baa au wanakoendaga, kwa hiyo nyinyi mnaweza kwenda pale ili mjue kitakachoendelea,” chanzo chetu kiliwasiliana na OFM ambao walifika katika baa anayofanya kazi Prisila bila yeye kufahamu na baadaye Mariam akiwa na mpambe wake nao waliwasili.
Baamedi, Prisila akipokea kichapo kutoka kwa rafiki wa Mariam Mohamed kwa kula ujana na mume wa mtu.
Akiwa hatambui kama anafuatiliwa, Prisila pamoja na rafiki yake mmoja
ambaye hakufahamika jina lake, waliondoka eneo hilo na kwenda kupanda
daladala lililokuwa likielekea Njiro na kuteremka eneo la Nguzo moja.
Mariam naye aliondoka na kuchukua usafiri binafsi kwa ajili ya
kuwafuatilia wasichana hao huku nyuma yao wakiwa OFM.
Prisila aliingia katika nyumba moja
iliyokuwa na geti jeusi majira ya saa tatu na muda mfupi baadaye Mariam
na mpambe wake nao waliwasili na kuukuta mlango ukiwa wazi.Baada ya
kuingia ndani, waliwakuta wawili hao wakiwa katika mkao wa kimahaba na
mara moja Mariam akiwa na fimbo, alianza kumchapa mumewe aliyejaribu
kumsihi kwa kupiga magoti ili walimalize jambo hilo kwa mazungumzo.
Wakati mume akipigwa na mke, mpambe alikuwa akimpa kichapo cha maana
Prisila.
Mume wa mtu na baamedi kwa pamoja wakiwajibishwa kwa kuvunja amri ya sita.
Rasha hata hivyo, baadaye alifanikiwa kumnyang’anya fimbo mkewe huyo
na kuanza kutoa vitisho kwa OFM waliokuwa wakipiga picha za tukio hilo.
Akizungumza wakati wa sekeseke hilo, Mariam alisema amekuwa akimfumania
mumewe mara kwa mara akiwa na wanawake tofauti na mara zote huomba
msamaha.Ingawa hawajafunga ndoa, Mariam alisema alianza kuishi na mwanaume huyo tangu mwaka 2004 na kwamba maisha yao yametawaliwa na migogoro kutokana na ukware wa mumewe.
Kwa upande wake, Rasha alisema yupo tayari kuachana na mkewe ili awe huru na maisha yake.
Post a Comment