- Ibara ya 15 iliyokuwamo katika Rasimu ya Warioba ilisema: “Kiongozi wa umma wakati anapotekeleza shughuli za kiserikali, akipewa zawadi, zawadi hiyo itakuwa ni mali ya Jamhuri ya Muungano na ilitaka Bunge kutunga sheria itakayosimamia, pamoja na mambo mengine, thamani, kiwango, aina na uhifadhi wa zawadi kwa Jamhuri ya Muungano. Mbali na ibara hiyo, pia Ibara ya 16 iliyohusu ufunguaji akaunti nje ya nchi, imeondolewa.
Dar/Dodoma. Rasimu ya Katiba
inayopendekezwa iliyowasilishwa bungeni juzi, imeondoa Ibara 28 zikiwamo
zinazowataka viongozi wa umma kutopokea zawadi kwa manufaa yao binafsi
wala kufungua akaunti ya benki nje ya nchi pasipo sababu maalumu,
Mwananchi limebaini.
Ibara ya 15 iliyokuwamo katika Rasimu ya Warioba
ilisema: “Kiongozi wa umma wakati anapotekeleza shughuli za kiserikali,
akipewa zawadi, zawadi hiyo itakuwa ni mali ya Jamhuri ya Muungano na
ilitaka Bunge kutunga sheria itakayosimamia, pamoja na mambo mengine,
thamani, kiwango, aina na uhifadhi wa zawadi kwa Jamhuri ya Muungano.
Mbali na ibara hiyo, pia Ibara ya 16 iliyohusu ufunguaji akaunti nje ya
nchi, imeondolewa.
Ibara nyingine zilizoondolewa ni pamoja na ya 17
iliyopendekeza uwazi wa mali ikimtaka kiongozi wa umma kutangaza thamani
ya mali na madeni yake mara tu baada ya kupata uongozi.
Pia Ibara ya 129 iliyokuwa inawaruhusu wananchi
kumvua madaraka mbunge ambaye atashindwa kuwasilisha au kutetea kwa
dhati hoja zinazotokana na kero za wapigakura wake au ataacha kuishi au
kuhamisha makazi yake kutoka eneo la jimbo la uchaguzi kwa zaidi ya
miezi sita bila sababu za msingi imeondolewa.
Ibara 28 zilizoondolewa
15. (1) Kiongozi wa umma wakati
anapotekeleza shughuli za kiserikali, akipewa zawadi, itakuwa ni mali ya
Jamhuri ya Muungano na ataiwasilisha kwa Katibu Mkuu Kiongozi kupitia
kwa katibu mkuu wa wizara au kiongozi wa taasisi ya Serikali
inayohusika, akiainisha:
(a) aina ya zawadi; (b) thamani ya zawadi; (c) sababu ya kupewa zawadi; na (d) mtu au mamlaka iliyotoa zawadi hiyo.
(2) Neno “zawadi” kama
lilivyotumika katika ibara hii linajumuisha kitu chochote chenye thamani
atakachopewa kiongozi wa umma katika utekelezaji wa shughuli za umma.
(3) Bunge litatunga sheria
itakayosimamia, pamoja na mambo mengine, thamani, kiwango, aina na
uhifadhi wa zawadi kwa Jamhuri ya Muungano.
16. Kiongozi wa umma-
(a) Hatafungua au kumiliki akaunti ya benki nje ya Jamhuri ya Muungano isipokuwa tu kwa namna ambayo sheria za nchi zinaruhusu; na (b) hataomba au kupokea mkopo au faida yoyote kwa namna au mazingira ambayo yanashusha hadhi au heshima ya utumishi wa umma.
17.-(1) Kiongozi wa umma
atalazimika kutangaza na kuwasilisha, ndani ya siku thelathini baada ya
kupata uongozi na baada ya kuacha uongozi, mali na thamani yake na
madeni yake katika Tume ya Maadili ya Uongozi na Uwajibikaji.
chanzo; mwananchi.
chanzo; mwananchi.
Post a Comment