Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

KWA NINI WANIGERIA WANAKIMBIZA KWENYE TELEVISHENI?

KATIKA siku za hivi karibuni, imekuwa kawaida kwa vituo vya televisheni vya Bongo kupiga sana video za muziki za wasanii wa Kinigeria kuliko hata za wazawa.

 
Mkali wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul, 'Diamond Platnumz'.
Kila kukicha wasanii wa Nigeria wanazidi kuongezeka na kazi zao zinazidi kuwa nzuri. Mfano wa wasanii waliochipukia juzijuzi na kupata umaarufu mkubwa ni Runtown na ngoma yake Gallardo, Pakorant na ngoma yake Girlie-O, mwanadada Yemi Alade anayezidi kubamba na ngoma yake ya Johnny, Chidinma na ngoma yake ya Oh Baby aliyomshirikisha Mr Flavour na wengine kibao.
Swali la kujiuliza ni kwa nini Wanigeria waingie katika gemu na kupata mafanikio makubwa hata katika nchi kama Tanzania wakati wasanii wa hapa hawatambuliki kihivyo nje ya mipaka ya Bongo?
Ni nadra kwa nyimbo za wasanii wa Kibongo kutambulika hata katika levo ya Afrika Mashariki tu, kwa nini inakuwa hivi? Ni wasanii wachache sana wa nyumbani ndiyo angalau ngoma zao zinapigwa kimataifa.
 
Mkongwe wa Bongo Fleva, Ambwene Yessaya 'AY'.
Nimeshuhudia angalau ngoma za Diamond, Shetta, AY na Linah zikipigwa kwenye levo za kimataifa lakini wengine wengi zinaishia hapahapa Kibongobongo. Je, nani wa kulaumiwa? Wasanii wenyewe au mameneja wanaosimamia kazi zao?
Nigeria inaongoza kiuchumi barani Afrika kwa sasa hivyo hata mzunguko wa fedha kwao ni mkubwa. Matajiri wengi wamewekeza katika muziki na unawalipa vizuri, mfano angalia mafanikio kupitia muziki waliyoyapata wasanii wakongwe kama 2 Face Idibia, P- Square, D Banj, Wiz Kid, Davido na wengine wengi.
Upande wetu Afrika Mashariki kiukweli tunajitahidi kufika levo hizo lakini soko la sanaa kwa upande huu bado lina shombo ya ugeni, hata wasanii watakaojaribu kutoka na uongozi wao, wengi huishia kutapeliana na kulumbana baada ya mafanikio kiduchu wanayoyapata, mwisho wasanii wanavunja uhusiano baina yao na uongozi uliowatoa.
 
Linah Sanga.
Wote tunalijua hilo na limekuwa likijirudia miaka nenda miaka rudi. Kwa ushauri wangu, kila msanii atakayesainishwa kwenye lebo yoyote ya muziki apewe mkataba uliopangilika na kuonesha maslahi yote atakayoyapata wakati wa mkataba huo.
Msanii ahakikishiwe mkataba sio wa chini ya miaka miwili, ili kumhakikishia kazi katika miezi 24 hivyo.
Uongozi usipende kuwahi maslahi tu, uhakikishe  unamkatia msanii bima ya afya kuepusha udhalilikaji wa kuombana michango ya matibabu au safari. Sote tunaelewa,sanaa yetu haina hela kama ya Wanigeria lakini tukianza kuaminiana kikazi huku tunapoanzia, basi hapo baadaye sanaa itakuwa inaingiza fedha nyingi kuliko sheria au fani nyingine.

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright BONGO HABARI
Back To Top