Hali
katika kampini ya RJ inayoongozwa kwa ubiya kati ya Vicent Kigosi (
Ray) na Blandina Chagula 'Johari', inazidi kuwa tete kwa kile
kinachoelezwa kuwa johari hataki kufanya kazi pamoja na 'mke mwenza'
Chuchu Hans.
Chanzo
hicho ambacho kipo karibu na wasanii hao kilisema kuwa mwezi mmoja
uliopita Johari na Chuchu, walikuwa katika kuelekea kuelewana ambapo
johari, alishakubali yaishe kuwa Ray wake ameshapokonywa na mtoto huyo
wa Kitanga .
Mnyetishaji
huyo aliendelea kusema kuwa baada ya Johari kuwa katika hali hiyo,ndipo
Chuchu alipoanza kutanua makucha yake ndani ya kampuni kwa kujifanya ni
mmoja kati ya wakurugenzi wakati ukweli haupo hivyo.
Chanzo
hicho kilizidi kusema kuwa imefikia hatua Chuchu, kaanza kutoa amri kwa
wafanyakazi wa kampuni hiyo bila ya kupata kibali kutoka kwa
wakurugenzi waasisi ambao mtaji wao unadaiwa kutokana na Johari
'kumpiga' changa la macho mfanyabiashara maarufu kutoka mkoani Mbeya.
Mpashaji
huyo alizidi kusema kuwa bifu liliibuka upya mkoani Dodoma, ambako Ray
na Johari walikwenda katika ziara ya Kilimanjaro Music Awards Tour, na
mashabiki wao kuwataka wapande jukwaani kwa pamoja.
Mtoa
habari hiyo alisema kuwa kuwa kutokana na hali hiyo, ndipo Chuchu
alipoanzisha bifu la chinichini lililopelekea hadi sasa kwenye kampuni
hiyo kuzuka mtafaruku mkubwa huku Johari, akitaka kujitenga kabisa na
Ray lakini kinachomkwamisha ni pesa zake nyingi alizowekeza.
Inadaiwa
kuwa Johari amekuwa mkali sana sasa hivi akimtaka mkurugenzi mwenzake
Ray, wagawane kila kitu mpaka nguo za ndani walizonunua kwa pesa za
kampuni yao hiyo.
Katika
kufuatilia habari hizo ili kupata ukweli kuhusiana na timbwili hili
mwanahabari wetu aliwasaka wote kwenye simu zao za mkononi, lakini wote
hawakutaka kutoa ushirikiano kwa kile walichokieleza kuwa wapo bize na
maswala binafsi.
Post a Comment