Mastaa Wema Sepetu na Nasibu Abdul ‘Diamond’ wakiwa kwenye pozi la kimahaba
Hilo liliibuka Suzi mjengoni katika kipindi cha maswali na majibu
ambapo Mbunge wa Jimbo la Mchinga, Saidi Mtanda alitaka kujua hatua
zilizochukuliwa na serikali katika kukabiliana na tabia za watu maarufu
kupiga picha zisizo na maadili kisha kuziweka mtandaoni.Katika kujibu swali hilo, Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Juma Nkamia alisema: “Tunajitahidi kuhakikisha wanaofanya hivyo wanachukuliwa hatua stahili ili kukabiliana na matendo hayo ambayo ni kinyume na maadili.”
Staa Nasibu Abdul ‘Diamond’ akiwa kwenye pozi lenye utata.
Katika kuonesha kutoridhika na majibu ya waziri, Mheshimiwa Mtanda
alipopewa nafasi aulize swali la nyongeza alisema: “Mheshimwa spika
nahisi swali langu halijajibiwa ipasavyo. Nilichotaka kujua ni hatua
ambazo zimechukuliwa kwa baadhi ya watu mastaa kama vile Wema na Diamond
ambao hupiga picha zao zisizofaa kisha kuziweka mtandaoni.”Kufuatia swali hilo, Nkamia alisimama na kujibu kwamba, serikali imeweka mikakati na njia sahihi za kukabiliana na tabia hiyo na kwamba wale ambao watabainika watachukuliwa hatua zinazostahili.
“Mheshimiwa kuhusu hizi picha za juzi zilizosambaa mtandaoni, tunazifuatilia kujua zimeanzia wapi na taarifa zake zikoje kwani hata mimi bado sijaziona ila tutachukua hatua tutakapobaini zilikotokea.”
Post a Comment